Wajiunga CHADEMA kufukuzia udiwani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]16 FEBRUARY 2012[/h][h=3][/h]

Na Bryceson Mathias, Morogoro

BAADHI ya watu wameanza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, ili kufukuzia nafasi ya udiwani iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo,marehemu Tusekile Mwakyoma.

Kasi ya kujiunga na CHADEMA ilianza kujitokeza hivi karibuni, baada ya chama hicho kutangaza sifa za mtu
anayetaka ateuliwe kugombea nafasi hiyo

Habari zilizilifikia gazeti hili mkoani hapa, zinadai kuwa baada ya CHADEMA kumaliza msiba, iliweka wazi sifa za mtu atakayeteuliwa na chama hicho ili kugombea nafasi hiyo .

“Tumebaini kasi kubwa ya waliokuwa si wananchama wa CHADEMA, imeongozeka kwa kasi, baada ya
chama kutangaza sifa za mtu anayefaa kuteuliwa na kugombea udiwani, lakini wengi hawana lengo la kuwatumikia wananchi ila cheo ,” alisema mzee aliyekataa jina lake lisitajwe gazetini.

Majina manane ya waliotajwa kuchukua fomu za chama hicho ni Bw. Peter Chengula, Bw. Pangrasi Kahinga, Bw. Lukasi Mwakambaya, Bw. Nassoro Manyama, Bw. Joshua Mshigati, Bw. Weliimo Lyimo, Bw. Mrisho Mohamed, na
Christian Seif.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Bw. Yusufu Mtamatale Mbaga alipoulizwa kwamba inadaiwa katika kundi hilo
kuna mamluki waliojiunga kwenye chama ili kuwavurugia uchaguzi

Marehemu Bi. Mwakyoma (28) alifariki Januari mosi, mwaka huu, baada ya kuchomwa kisu chini ya titi.



 
Sio CCM pekee ndio chama hata Chadema ni chama cha kuongoza wananchi vijijini
 
CHADEMA siku zote kiko makini. Kitakuwa makini katika suala hilo na mengine yote. Ni wakati mwafaka wa kuonesha kuwa ni serikali mbadala, yenye kila sifa mbadala, za kupewa dhamana na kuongoza dola. Bila shaka yoyote uongozi kuanzia ngazi ya chini, watahakikisha chama kinapata mrithi anayestahili nafasi iliyoachwa na mwana mama yule mpiganaji. Asante.
 
Naomba Chadema kiwe makini zaidi kwa wanachama wapya hasa pale wanapotaka kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama. Isije kutokea kama ilivyotokea Arusha kwa
madiwani.
 
Mcheza ngoma ya kijadi hawezi cheza western music mpaka afundwe. wataonekana kwenye hoja kama wanatoka CCM
 
Back
Top Bottom