Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,163
- 37,801
Hicho KIJIJI cha watu, wamekusanyika wanamskiliza MTAALAMU wa tiba za jadi. Jirani ya huo Mzunguko, kuna kakibanda kangu ka mradi bubu wa wazalendo.
Mtaalamu ameweka Katikati ya KIJIJI kitu mfano wa kapu kisha akafunika na shuka, kwa maelezo anasema humo kuna mnyama wa ajabu zaidi ya NYOKA WA VICHWA VITATU ambaye watu wamezoea kumuona.
Mara kwa mara huwa anatishia hadhira yake kuwa watoto wasikae mbele, eti yeye hajui nini MNYAMA huyo atafanya endapo atafunguliwa. Cha ajabu sasa, hasemi mnyama wake ni nani? Na kwa nini kamleta katika kadamnasi kamtoa wapi hasemi?
Muda wote anapiga porojo zake, huku pia anahamasisha uuzaji wa dawa km za kupata mke, kupata mume, dawa za biashara, dawa za utajiri, n.k. Masikitiko makubwa ni pale ambapo mpk Jua linazama, hakuna mdudu wala mnyama aliemtoa watu wa muone!
Na hii si mara moja, mara kwa mara huyu bwana na msaidizi wake, wanawachukulia watu chenji zao kiulaini.
Hawa wajinga kwa nini hawaishi? Nini kifanyike ili waelimika? Ni kweli mabasi ya mikoani yanakuja na watu hawa?