Wajibu wa Biashara/Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility)

Wajibu wa Biashara/Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibility)

The Consult

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
220
Reaction score
252
1153838

Uwajibikaji kwa Jamii ama "Corporate Social Responsibility" ni kitendo cha kampuni kuwajibika (morally responsible) katika masuala yanayohusu jamii, hususani mahala ambapo hiyo kampuni huendesha shughuli zake. Dhana ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii ina upana kwa kiasi fulani, wakati mwingine, uwajibikaji wa kampuni hutafsirika kwa makundi yafuatayo;
  • Wamiliki (Owners) wajibu mkubwa wa kampuni ni kuhakikisha inaleta tija kwa wamiliki wake kupitia uingizaji wa faida na ukuaji kimasoko.
  • Wateja (Customers), kufanikiwa au kufeli kwa kampuni kwa kiasi kikubwa kupo mikononi mwa wateja wake, ikiwa wateja watanunua bidhaa za kampuni, basi kampuni itafanya vizuri, kinyume na hapo itadondoka. Kwa mantiki hii, ni wajibu wa kampuni kuhakikisha inawapatia wateja wake kile wanachohitaji.
  • Wadai (Creditors) hawa ni watu ambao wameikopesha kampuni aidha fedha au vifaa kwa kipindi fulani cha muda, ili kuiwezesha kampuni kufanya shughuli zake. Wajibu wa kampuni ni kuhakikisha inarudisha mikopo kwa wakati ili itakapohitaji tena baadae iweze kupatiwa
  • Wafanyakazi (Employees), hawa ndio wazalishaji wa bidhaa na huduma za kampuni. Kampuni ina wajibu wa kuhakikisha inawalipa vizuri, inawatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia kazi n.k
  • Serikali (Government) kampuni ina wajibu wa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka katika uendeshaji wa shughuli za kibiashara (A business has to be a good citizen)
  • Jamii (Community) kampuni ina wajibu wa kuhakikisha jamii ina ishi katika mazingira safi na salama kwa kutatua matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii kama ukosefu wa maji, elimu n.k
UWAJIBIKAJI WA KAMPUNI KWA JAMII NA NAFASI YA ASASI ZA KIRAI (CSOs)

Kama nilivyoeleza hapo juu, kampuni ina wajibu wa kuhakikisha jamii (mahala ambapo kampuni inafanya shughuli zake) inaishi katika hali nzuri na salama. Katika kuhakikisha hili, kampuni nyingi za ndani na nje zimekuwa zikianzisha mifuko "funds, foundation" kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii. Kupitia mifuko hii, Asasi za Kiraia (CSOs) huweza pia kupata fedha kwa ajili ya kuzisaidia hizi kampuni katika kutimiza wajibu wao katika kuisaidia jamii kwenye utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Mifano ya kampuni ambazo zimeanzisha mifuko kwa ajili ya kusaidia jamii;
  • VODACOM FOUNDATION; hii foundation inasaidia wanawake na wasichana katika maeneo ya elimu, afya n.k. Kwa kiasi kikubwa imekuwa ikishirikiana na Asasi za Kirai katika kutekeleza malengo yake. Mpaka sasa imeweza kufadhili miradi 120 yenye thamani ya Shilingi bilioni 14
  • TIGO-CSR ; hili ni eneo chini ya kampuni ya TIGO, ambalo limejikita katika kusaidia watu katika nyanja za elimu, biashara na teknolojia
  • DANGOTE FOUNDATION; huu ni mfuko ulio chini ya kampuni ya DANGOTE GROUP wenye lengo la kusaidia jamii katika kukabiliana na maradhi, lishe duni nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla. Mpaka sasa imetoa kiasi cha Dola Milioni 100 kusaidia watu mbalimbali Afrika
  • FORD FOUNDATION, UEFA Foundation for Children, CISCO Foundation Global Impact Cash Grants n.k
Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia jamii kutoka kwenye mifuko ya kampuni hizi, huweza kuambatana na Taarifa (Calls for Proposals) au pasina taarifa. Hivyo basi ikiwa wewe kama NGO unahitaji kuisaidia jamii, kwa kutumia fedha kutoka kwenye Mifuko ya Makampuni mbalimbali, ni vyema kwanza ukatambua malengo yao/vipaumbele vyao katika wakati husika (their current strategic objectives/priorities) kabla ya kuwapelekea andikolako la mradi.

Aksante

The Consult; +255 719 518 367

E-mail; theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania

Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising Management
 
Corporate Social Responsibility (CSR) kwa kiasi kikubwa husaidia kujenga 'BRAND" ya biashara yako, ambayo in a long-run itakuletea faida kubwa.
 
Back
Top Bottom