Wajibika ili watuhumiwa wa Escrow wawajibike

Joined
Jul 17, 2013
Posts
30
Reaction score
36
Ni vyema watanzania tukaonyesha msisitizo wetu kwa wabunge na utawala kwamba suala la uwajibikaji katika hii scandal ya ESCROW haikwepeke.

Tunawasii wote msaini petition hii https://secure.avaaz.org/en/petitio...UWAJIBIKAJI_KAMILI_UNATENDEKA_NA_PESA_ZA/edit ili msimamo wetu ueleweke kwamba hatuna tena urafiki na wizi/wezi wa mali za umma?
Tubadilike tuwe na utamaduni wa kuwaonyesha hisia zetu wale wanaofanya makosa kwenye ofisi za umma na kupelekea maendeleo yetu kama taifa kuchelewa.

KWA NINI BASI ILI SUALA NI MUHIMU KWETU WATANZANIA

Sisi wananchi wa Tanzania:

Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na Rais wa JMT kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa hali ya juu unafanyika na wahalifu waliokwapua pesa za umma za Tegeta Escrow mwezi wa 12, mwaka 2013 wanazirudisha mara moja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

  • Uwajibikaji tunaotaka kuuona ni pamoja na:

  • Wahusika wote wakiwa ama watumishi wa serikali au mawaziri wafukuzwe kazi au kujiuzulu mara moja.
  • DPP afungue mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa uhalifu huu na wanufaika wote wa pesa za Tegeta Escrow.
  • Pesa zirudishwe hata ikitakiwa kwa kuwafilisi wanufaika wa pesa hizi.

  • Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea uwazi na uwajibikaji nchini kwetu. Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linaangamiza taifa na wananchi na kunachangia kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Tunataka uwajibikaji kamili na pesa za Tegeta Escrow ​
Zirudishwe mara moja ​
KWA SABABU:- Kutokana na taarifa tulizopokea kutoka vyanzo vinavyoaminika kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG); imedhihirika kuwaTANESCO ilikuwa na haki ya kulalamika kuwa ilikuwa ikitozwa na IPTL gharama za uendeshaji (capacity charges) zaidi ya kile kilichokuwa stahili (over charging). Gharama za kukotoa ‘capacity charges' zilitokana na gharama za mwanzo za uwekezaji pale IPTL, kwa makusudi IPTL iliziongeza gharama hizo kinyume na ukweli na mkataba wake na Tanesco.

KWA SABABU:- Account ya Tegeta Escrow ilifunguliwa mwaka 2006 katika Benki Kuu (BoT) kwa mujibu ya maamuzi ya mahakama ya usuluhishi iliyoshauri kuwa badala ya kulipwa IPTL pesa zile zitunzwe na Benki kuu (escrow account) hadi pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi na mahakama ya kimataifa ICSID. Ufumbuzi huu ni uamuzi wa ama kukubali kiwango cha capacity charges walichokuwa wakidai IPTL au kukataa na kutumia kiwango ambacho Tanesco walikuwa wakidai. Kwa mazingira ya kutatanisha pesa zote za Escrow zililipwa kwa IPTL mwezi wa 12, mwaka 2013 kabla ya hukumu ya ICSID iliyotelewa mwezi wa 2, mwaka 2014. Hivyo ulipaji huu ulikuwa kinyume cha sheria na makubaliano ya Escrow.
(Facts on IPTL deal ahead of the tabling of escrow scam report - National - thecitizen.co.tz )

KWA SABABU:- Ulipaji huu ulio kinyume na sheria, na ulifanywa huku wahusika kutoka serikalini wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, maafisa wa TANESCO, BoT, TRA wakiwa na ufahamu na kushiriki katika mchakato huu wa kihalifu.

KWA SABABU:- Uchunguzi wa PCCB umepata wanasiasa wakiwemo wabunge, mawaziri, majaji na viongozi wengine wa serikali wakishirikishwa katika ‘mgao' wa fedha hizi tena kwa viwango vya kutisha hadi mabilioni.
KWA SABABU: - Bodi ya shirika la TANESCO haikutimiza wajibu wake na kusababisha ulipaji wa fedha za Tegeta Escrow kinyume na utaratibu, makubaliano na sheria na hivyo kuisababishia TANESCO hasara ya shilingi 321 bilioni .

UWAJIBIKAJI KAMILI TEGETA ESCROW!

​
UPDATE

Report ya PAC ufisadi wa #TegetaEscrow https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/764613-uwasilishaji-wa-ripoti-ya-pac-kuhusu-tegeta-escrow-account.html

Kwa niaba ya wazalendo wote Change Tanzania
 
Pamoja na yote haya, wabunge waondoe jazba katika kushughulikia suala hili.
Wakati mwingie mambo mazito kama hayo yanahitaji extra push, ni kweli wakumbuke wajibu wao ila wasihache kuwa wakali, !!! kama ni wakati wa kuwa wakali ni sasa, wizi umefanyika sana na kujirudia rudia sana
 
Aaamin nawaambia serikali imeshindwa katika hili kwa kukalia report ya CAG bila kuifanyia kazi. Mahakama nayo imeshindwa kazi mara zote kwa kushindwa kuwawajibisha mafisadi. Bunge nalo sasa linaanza kudhihirisha kushindwa kuwawakilisha wananchi. Tumaini pekee ni kwa wananchi wenye uchungu kuiwajibisha mihimili yote mitatu kwa njia iwayo yote ile. Kwahili tukiliacha liendelee hivi dunia itatushangaa na zaidi watoto wetu hawatatuelewa. Mimi naanza kuchukua hatua na naomba Mwenyezi Mungu Nisaidie.
 
Nakubali hoja LAKINI haitoshi!!! Its very easy kuona kwamba tunachezewa mchezo wa hide and seek kama kweli changeTANZANIA mnataka kutusaidia watanzania PLEASE PLEASE PLEASE ratibuni maandamano ya amani. Kuna watu wengi wako tayari kuingia barabarani tatizo hawajui nani awashike mikono...so again please saidia kuonyesha njia ya wapi pa kuanzia sisi tutafuata.
 
Last edited by a moderator:
Change Tanzania hii kusign petition online naona kama ni uzungu uzungu sana ambao hauna direct impact kwetu.
Itisheni maandamano dar, mwanza, arusha mbeya watu waje tufanye peaceful demonstrations.
Japo hili ni wazo zuri theoretically, sijui lina nguvu kiasi gani realistically!
 
Last edited by a moderator:
Wananchi tunatakiwa kuwa wakali, mambo mengi ya ovyo yanatokea tunahacha tu yanapita, ni vyema ku saini hii petition ili kuonyeshe msimamo wetu kama wananchi.
Tusisubiri wajiwajibishe maana wanaweza wasifanye hivyo, tuweke msukumo ili wawajibike

Aaamin nawaambia serikali imeshindwa katika hili kwa kukalia report ya CAG bila kuifanyia kazi. Mahakama nayo imeshindwa kazi mara zote kwa kushindwa kuwawajibisha mafisadi. Bunge nalo sasa linaanza kudhihirisha kushindwa kuwawakilisha wananchi. Tumaini pekee ni kwa wananchi wenye uchungu kuiwajibisha mihimili yote mitatu kwa njia iwayo yote ile. Kwahili tukiliacha liendelee hivi dunia itatushangaa na zaidi watoto wetu hawatatuelewa. Mimi naanza kuchukua hatua na naomba Mwenyezi Mungu Nisaidie.
 
Kuratibu maandamano sio shida, kumbuka ni maandamano yetu sisi sote kama wananchi, hivyo basi kusaini hii petition ni kuonyesha ummoja wetu,
Kwa nchi wanazojari maendeleo yao vitu kama petition is a key kuonyesha msimamo wao, sisi tunakapokusanya sahihi za kutosha tunaweza ziwasilisha kunakohusika kwa maandamano
Nakubali hoja LAKINI haitoshi!!! Its very easy kuona kwamba tunachezewa mchezo wa hide and seek kama kweli changeTANZANIA mnataka kutusaidia watanzania PLEASE PLEASE PLEASE ratibuni maandamano ya amani. Kuna watu wengi wako tayari kuingia barabarani tatizo hawajui nani awashike mikono...so again please saidia kuonyesha njia ya wapi pa kuanzia sisi tutafuata.
 
Lets put our hands together and "gun them down"
 
Nani amwajipishe mwenzake kama wote wanahusika !

Sisi kama wananchi tunaweza kuwawajibisha, hakuna serikali inayokaa madarakani bila UKUBARI wa wananchi, tuki saini na kuonyesha ummoja watawajibika tu, Nchi zilizoendelea zinatumia petition kama ishara ya kuonyesha ukubwa wa jambo, tusaini kwa nguvu zote kuonyesha msimamo wetu.
Ni wakati wa sisi kuamua mambo ya nchi yetu kwa kutumia njia za ki democrasia, Kumbuka hii petition iko kwenye public domain
 
Ni vyema watanzania tukaonyesha msisitizo wetu kwa wabunge na utawala kwamba suala la uwajibikaji katika hii scandal ya ESCROW haikwepeke.

Tunawasii wote msaini petition hii https://secure.avaaz.org/en/petitio...UWAJIBIKAJI_KAMILI_UNATENDEKA_NA_PESA_ZA/edit ili msimamo wetu ueleweke kwamba hatuna tena urafiki na wizi/wezi wa mali za umma?
Tubadilike tuwe na utamaduni wa kuwaonyesha hisia zetu wale wanaofanya makosa kwenye ofisi za umma na kupelekea maendeleo yetu kama taifa kuchelewa.

KWA NINI BASI ILI SUALA NI MUHIMU KWETU WATANZANIA

Sisi wananchi wa Tanzania:

Tukiwa ni wapiga kura wa majimbo mbalimbali nchini Tanzania, tumechukua jukumu leo kutoa wito kwa wabunge na Rais wa JMT kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa hali ya juu unafanyika na wahalifu waliokwapua pesa za umma za Tegeta Escrow mwezi wa 12, mwaka 2013 wanazirudisha mara moja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

  • Uwajibikaji tunaotaka kuuona ni pamoja na:

  • Wahusika wote wakiwa ama watumishi wa serikali au mawaziri wafukuzwe kazi au kujiuzulu mara moja.
  • DPP afungue mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa uhalifu huu na wanufaika wote wa pesa za Tegeta Escrow.
  • Pesa zirudishwe hata ikitakiwa kwa kuwafilisi wanufaika wa pesa hizi.

  • Hii ni sehemu muhimu ya wajibu wetu kama raia waaminifu, wenye nia njema ya kuchangia mawazo bora yatakayotuletea uwazi na uwajibikaji nchini kwetu. Kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linaangamiza taifa na wananchi na kunachangia kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Tunataka uwajibikaji kamili na pesa za Tegeta Escrow ​
Zirudishwe mara moja ​
KWA SABABU:- Kutokana na taarifa tulizopokea kutoka vyanzo vinavyoaminika kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG); imedhihirika kuwaTANESCO ilikuwa na haki ya kulalamika kuwa ilikuwa ikitozwa na IPTL gharama za uendeshaji (capacity charges) zaidi ya kile kilichokuwa stahili (over charging). Gharama za kukotoa ‘capacity charges' zilitokana na gharama za mwanzo za uwekezaji pale IPTL, kwa makusudi IPTL iliziongeza gharama hizo kinyume na ukweli na mkataba wake na Tanesco.

KWA SABABU:- Account ya Tegeta Escrow ilifunguliwa mwaka 2006 katika Benki Kuu (BoT) kwa mujibu ya maamuzi ya mahakama ya usuluhishi iliyoshauri kuwa badala ya kulipwa IPTL pesa zile zitunzwe na Benki kuu (escrow account) hadi pale mgogoro utakapopatiwa ufumbuzi na mahakama ya kimataifa ICSID. Ufumbuzi huu ni uamuzi wa ama kukubali kiwango cha capacity charges walichokuwa wakidai IPTL au kukataa na kutumia kiwango ambacho Tanesco walikuwa wakidai. Kwa mazingira ya kutatanisha pesa zote za Escrow zililipwa kwa IPTL mwezi wa 12, mwaka 2013 kabla ya hukumu ya ICSID iliyotelewa mwezi wa 2, mwaka 2014. Hivyo ulipaji huu ulikuwa kinyume cha sheria na makubaliano ya Escrow.
(Facts on IPTL deal ahead of the tabling of escrow scam report - National - thecitizen.co.tz )

KWA SABABU:- Ulipaji huu ulio kinyume na sheria, na ulifanywa huku wahusika kutoka serikalini wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, maafisa wa TANESCO, BoT, TRA wakiwa na ufahamu na kushiriki katika mchakato huu wa kihalifu.

KWA SABABU:- Uchunguzi wa PCCB umepata wanasiasa wakiwemo wabunge, mawaziri, majaji na viongozi wengine wa serikali wakishirikishwa katika ‘mgao' wa fedha hizi tena kwa viwango vya kutisha hadi mabilioni.
KWA SABABU: - Bodi ya shirika la TANESCO haikutimiza wajibu wake na kusababisha ulipaji wa fedha za Tegeta Escrow kinyume na utaratibu, makubaliano na sheria na hivyo kuisababishia TANESCO hasara ya shilingi 321 bilioni .

UWAJIBIKAJI KAMILI TEGETA ESCROW!
​

Kwa niaba ya wazalendo wote Change Tanzania

Asante Dada Yetu...!!! Tupo Pamoja katika Hili!!!!! Uwajibikaji Ni Muhimu Tusiache Wapite Hivi Hivi..!! Hatuja Jenga Segerea kwa ajili ya Wezi Wa Kuku Tuuu..!!! Hata Hawa Shurti Wasulubiwe.
 
Ushindi ni wetu sote, tujenge umoja ili tuwe na team bora kama wananchi, wananchi tukiwa imara pamoja huu wezi na matumizi mabaya ya ofisi yatapungua
Asante Dada Yetu...!!! Tupo Pamoja katika Hili!!!!! Uwajibikaji Ni Muhimu Tusiache Wapite Hivi Hivi..!! Hatuja Jenga Segerea kwa ajili ya Wezi Wa Kuku Tuuu..!!! Hata Hawa Shurti Wasulubiwe.
 
Well hii kitu iko sawa. Na imewalenga Watanzania wote haswa wale ambao hawapo nchini lakini wana 'access' na mitandao waweze kupaza sauti katika yale yanayowakwaza katika Nchi yao.

Ukiachana na Petition hii online pia zimefanyika juhudi za ziada na karatasi zimesambazwa nchi nzima kuwahamasisha Watanzania waamke na wawe na uwezo wa kusimamia na kuwawajibisha wote waliowapa dhamana ya kutawala.

Change Tanzania hii kusign petition online naona kama ni uzungu uzungu sana ambao hauna direct impact kwetu.
Itisheni maandamano dar, mwanza, arusha mbeya watu waje tufanye peaceful demonstrations.
Japo hili ni wazo zuri theoretically, sijui lina nguvu kiasi gani realistically!
 
Kuratibu maandamano sio shida, kumbuka ni maandamano yetu sisi sote kama wananchi, hivyo basi kusaini hii petition ni kuonyesha ummoja wetu,
Kwa nchi wanazojari maendeleo yao vitu kama petition is a key kuonyesha msimamo wao, sisi tunakapokusanya sahihi za kutosha tunaweza ziwasilisha kunakohusika kwa maandamano

Tunatakiwa kuwaeleza DONORs kwa sasa hatuhitaji PESA zao mpaka kwanza WATAWALA wetu watueleze pesa zetu ziko wapi.Na waliozichota ndiyo wafaidika wakuu kwenye fedha za wafadhili.
 
Ni wazo zuri na labda tukiweza kupata sahihi za kutosha ndani ya wiki hii tunaweza kuwatumia mahisani na kuwaonyesha kwa vielelezo kile tunachotaka hivyo kusaidia kuongeza presha au msukumo katika kuhakikisha uwajibikaji kamili unafanyika
 
Back
Top Bottom