Wajeshi 300 waja juu ,wakiwemo usalama wa Taifa na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wajeshi 300 waja juu ,wakiwemo usalama wa Taifa na polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Apr 20, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Askari wastaafu Z’bar wajipanga kudai pensheni

  na Mwanne Mashugu, Zanzibar

  ASKARI wastaafu Zanzibar wameamua kuitisha mkutano wa hadhara kupanga mkakati wa pamoja baada ya kukwama kulipwa pensheni ya muda wa miezi sita na serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Askari hao wapatao 300 ni kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Usalama wa Taifa pamoja na askari polisi, ambao wanaishi katika mikoa mitano ya Zanzibar baada ya kulitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 30 kabla ya kustaafu.

  Wakizungumza na waandishi wa habari Kikwajuni mjini Zanzibar, walisema mkutano huo wa hadhara umelazimika kuitishwa baada ya kuona maofisa wa Hazina Zanzibar wamekuwa wakiwapiga danadana kuhusu suala la malipo yao.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, askari mstaafu wa JWTZ, Juma Omar Juma, alisema Wizara ya Fedha ya Muungano imekuwa na utaratibu wa kuwapatia mafao yao kwa kutuma fedha Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar kila baada ya miezi sita.

  Hata hivyo, alisema mwaka huu wameshangazwa baada ya kujitokeza tatizo la askari wengine kulipwa na wengine kuelezwa fedha zao hazijaja wakati wamestaafu mwaka mmoja.

  Alisema hivi sasa wanalazimika kuishi katika mazingira magumu kwa vile baadhi ya familia zimeanza kuingia katika ugomvi mkubwa baada ya kutiliwa shaka na wake zao kuwa wamepokea mafao, lakini wamehonga.

  Alisema baada ya tatizo hili kujitokeza waliamua kutuma ujumbe maalumu kufuatilia Tanzania Bara kupitia umoja wa askari wastaafu (UMAWA) na kuelezwa kuwa hundi zimeshatumwa Zanzibar.

  “Waandishi tunaomba mtusaidie hivi sasa tuko njia panda hatujui tufanye nini, ndiyo maana tumeamua kupeleka malalamiko yetu Ofisi ya Waziri Kiongozi kwa vile tuko katika mazingira magumu,” alisema Juma Omar.

  Alifahamisha kwamba chimbuko la kufuatilia mafao yao lilitokana na kituo cha matangazo cha televisheni ya taifa TBC1 kuwataka wafike Hazina kwa malipo kwa vile tayari taratibu za kulipwa pensheni zao zimekwisha kukamilika.

  Hata hivyo, alisema baada ya kuripoti Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar Januari 26 mwaka huu walitakiwa warudi Februari 5, lakini baada ya kufika wakatakiwa warudi Machi mwaka huu.

  Akifafanua zaidi alisema baada ya kuripoti wametakiwa warudi nyumbani na waendelee kuwa na subira hadi hapo matangazo yatakapotolewa tena kupitia Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ).

  Hata hivyo, alisema kinachosikitisha baadhi ya askari wastaafu wanalazimika kusafiri kutoka kisiwani Pemba kufuatilia mafao yao kisiwani Unguja na hivyo kupata usumbufu mkubwa baada ya kuelezwa kuwa fedha zao hazijafika.

  “Kuna wastaafu wameazima nauli kwa malengo ya kurejesha baada ya kupata mkupuo wa miezi sita, leo unafika unaambiwa fedha zako hazijafika na unashuhudia mwenzio mliyestaafu mwaka mmoja akilipwa, ndio maana tumeamua kuitisha mkutano wa hadhara ili kulijadili kwa undani suala hili,” alisema askari mstaafu huyo.

  Alisema suala hilo ni zito kwa vile hivi sasa limeanza kuathiri baadhi ya askari wastaafu kwa kushimdwa kulipa madeni kutokana na kukopa bidhaa, zikiwemo vyakula kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara.
  ____________________________

  Hao ni WaZanzibari ambao hawana uswahiba na serikali ,wanataka kijulikane je WaTanganyika mnayaweza hayo ?
   
 2. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #2
  Apr 20, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  vipi kuhusu wastaafu wa iliyokuwa jumuia ya africa mashariki, walishalipwa?? wale wazee waliokuwa wanaandamana ikulu Kondolo anaenda kuwapooza!
   
Loading...