Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,467
- 7,258
BAADHI ya wakazi wa wilayani Ileje, Mkoa wa Mbeya, hawaifahamu sera ya afya ya mwaka 2007.
Katika sera hii inatamkwa kwamba wajawazito nchini watapewa huduma za afya bure.
Baadhi ya wajawazito wanaacha zahanati, vituo vya afya na hospitali wilayani mwao na kuvuka mpaka hadi nchini Malawi kufuata kinachoitwa ‘huduma bora.'
Kwa mfano, wajawazito kutoka kata za Bupigu, Itumba na Isongole wanakwenda Malawi kwa wingi ili waweze kujifungulia huko na kupata huduma nyingine za afya.
Lakini kutoka Isongole hadi Hospitali maarufu ya Chitipa, Malawi ni umbali wa kilometa 45; wakati umbali wa kwenda hospitali ya serikali ya Ileje ni kilomita tatu tu.
Mwanamke mkazi wa Kijiji cha Ikumbilo, Kata ya Chitete anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), anasema aliwahi kujifungulia Hospitali ya Chitipa na hadi sasa anapata matibabu yake huko.
Kuna nini katika Hospitali ya Chitipa nchini Malawi hadi wajawazito wakimbilie huko? Jibu analo Neema Mbughi mkazi wa Kijiji na Kata ya Bupigu.
"Pale Hospitali ya Chitipa hubebi chochote wakati unakwenda kujifungua. Hatuendi na madishi, karatasi za nailoni wala glovu. Kila kitu ni bure, hata chakula ambacho kimepikwa kama kimetoka nyumbani," anaeleza Neema.
Wilaya ya Ileje ina hospitali kubwa mbili; hospitali ya serikali mjini Ileje na ile ya misheni ya Isoko. Hizi ndizo hospitali ambazo zinategemewa kwa huduma ya uzazi.
Wanawake wapatao 27 waliohojiwa, pamoja na kutofautiana katika mambo mengine, wengi waliafikiana kuwa katika Hospitali ya Chitipa wauguzi wanatumia ‘lugha nzuri' inayompa matumaini mjamzito.
Sababu nyingine walizotaja ni kutotozwa fedha yoyote ikiwa ni gharama kwa kujifungulia hapo; kupewa dawa zinazohusiana na uzazi bila kulipia na kupewa chakula bure.
Hivi wanapitaje mpakani penye Idara ya Uhamiaji? Jibu unalopewa ni kwamba hawapiti mpakani kwenye ofisi za serikali. Wanapita vichochoroni ambako wanaita ‘njia za panya.'
Bali wakifika hospitalini Chitipa wanajieleza kuwa wanatoka vijiji vya ndani ya Malawi, wengine wakitaja hata ndugu zao na viongozi katika maeneo hayo kuthibitisha kuwa wanatoka humohumo
Neema anasema wanalazimika kusema kuwa wanatoka Malawi ili waweze kupata huduma za kliniki, mahali bora na bure pa kujifungulia na matibabu mengine.
Si wajawazito pekee wanaoingia Malawi kwa matibabu. Wananchi wengine huenda hospitali za Chitipa na Kameme kupata matibabu; tena bila kutozwa fedha zozote.
Henry Kayuni, mkazi wa Bupigu anasema licha ya kufuata matibabu na mahitaji mengine kama mafuta ya taa, mbegu za mahindi, sukari na mbolea, baadhi yao wanawapeleka pia watoto wao shuleni.
Anasimulia kwamba kujieleza kuwa unatoka Malawi kunasaidia hata kusomesha watoto nchini humo hadi darasa la saba.
"Baada ya hapo wanakuwa tayari wamejua vema Kiingereza; ndipo wanahamishiwa Tanzania na kuwaombea nafasi sekondari," anasema.
Lida Kibona wa Kijiji cha Itumba, anasema yeye alianza kupata matibabu bure katika Hospitali ya Chitipa hata kabla hajapata ujauzito na kwamba manesi na madaktari wanasikiliza na kujali sana wagonjwa.
Kuna kichocheo kingine kwa wananchi wa Tanzania kutibiwa Chitipa. Katika mahojiano nao Novemba mwaka jana walieleza, mmoja baada ya mwingine, kuwa ikitokea mama au mtoto akafariki dunia na wakati huo umejitambulisha kuwa unatoka Tanzania, basi mwili wa marehemu utasafirishwa hadi mpakani bila gharama yoyote.
Katika hospitali za mkoani Mbeya karatasi la kutandika wakati wa kujifugua linauzwa kwa sh 3,000, paketi ya glovu sh 2,000, beseni sh 3,000 na kama mjamzito amelazwa, basi hujitegemea pia kwa chakula.
Jane Kabuje, mkazi wa Kata ya Isongole anasema kuwa yeye ni mmoja wa wanawake wanaopata huduma za afya Chitipa nchini Malawi ingawa Hospitali ya Wilaya ya Ileje ipo ndani ya kata yake.
Mkazi wa Bupigu, wilayani Ileje, Amos Shimwela, anasema tatizo linalowakumba wakazi wa vijiji vya mpakani hadi kuamua kujitambulisha kama raia wa Malawi ni kutokana na kutopata huduma za afya nchini ambazo alisema ni ghali wakati nchini Malawi ni bure.
Naye mkazi wa Kijiji cha Bulambya, Joseph Kapange, anasema ni bora kujitambulisha kuwa ni raia wa nchi nyingine ili upate huduma, kuliko kung'ang'ania utokako ambako hupati huduma muhimu kwa afya yako.
Anasema wakati matibabu katika Hospitali ya Chitipa na huduma kwa wajawazito ni bure, nchini Tanzania bado wanatozwa fedha na wengi wanashindwa hata kulipa sh 500 ili kupewa kadi ya kumwona daktari.
Hata wanaomudu kulipa kiasi hicho cha fedha bado wanalazimika kununua dawa katika maduka nje ya hospitali.
Mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama Minga, anasema baadhi ya wanaume wamekuwa wakipeleka wake zao wajawazito katika Hospitali ya Chitipa miezi mitatu kabla ya kujifungua.
Anasema hii ni kwa tahadhari, kwa kuwa wanaishi mbali na hospitali hiyo; na kwamba hawataki kusubiri hadi wajawazito wazidiwe kwa sababu usafiri wa barabara si wa uhakika.
Hapa ndipo ilipofikia nchi yetu...aibu ya maisha,wananchi wanateseka mno hadi wanaenda kuponea nchi jirani...watawala wetu wako bize na ufisadi, kuhonga wapinzani ili wavuruge vyama vyao na kupanga mikakati ya kuwauwa baadhi yao kwa mabiliono ya pesa....!!