Wajasiriamali/wafanyabiashara na wafanyakazi sekta binafsi ndo raia wazalendo zaidi nchi hii Wathaminiwe

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,213
1,228
Wajasiriamali wadogo na wakubwa,

Wafanya Biashara ,ndogo za kati na kubwa

Na wafanyakazi wote sekta binafsi,

Ambao pesa yetu haitokani na bajeti ya serikali, and yet tunalipa kodi tena kwa kiwango kikubwa

Tunatunisha mifuko ya Pension houses ,Tuna toa ajira kwa wengine

Hatutegemei fungu lolote toka serikalini lakini Kila mwezi tunalipa mabilion ya pesa kama PAYE, VAT, SDL, Withholding taxes etc etc

Sisi ndo raia wa daraja la kwanza Tz, tusikilizwe, tukiwa na maoni yetu, tutatuliwe changamoto pale tunapo zionesha

tunapaswa kuwa wengi zaid, sisi ndo tunaojenga Uchumi wa nchi hii


Tunapaswa kutambua umuhimu wetu Lakin pia na serikali, na watumishi wa serikali watambue umuhimu wetu.

Napendekeza kuwe na siku maalumu ya kitaifa ya Sekta binafsi

Kama illivyo mei mosi, ambayo ni kama huwa inakuwa imehodhiwa na wafanyakaz wa sekta ya umma tu (Na ndo maana ombi kubwa huwa linakuwa nyongeza ya mshahara, na Rais huwa anasimama kama mwajir Mkuu) kitu ambacho kwa sisi wa sekta binafsi rais sio mwajiri bali ni regulator na msamiz Mkuu


Hivyo nadhan tunahitaj siku hii ambayo tutaitumia kuangazia changamoto za sekta binafsi, na kuangalia namna bora zaid ya kuiboresha.

Mwalimu wa sekta binafsi analipwa Million gross anakatwa kodi laki 3, TRA wanaipokea wanaipeleka hazina, hazina wanamlipa Mwalimu wa public sekta.(in theory)

So bila private sekta, hata serikali itakuwa mufilisi

Ni dhana iliyowazi ila inasahaulika kirahis sababu ina operate nyuma ya pazia na viongoz hawaioni, ndio sababu tuna baadhi ya viongoz ambao ukiwatazama ni kama hawaoni umuhimu wa sekta binafsi


Napendekeza siku ya mashujaa ,tarehe moja september iwe siku ya sekta binafsi pia

Wadau wa sekta binafsi ni Mashujaa wa nchi hii.
 
Mkuu wafanyakaz wa serikali ndio nguzo kuu ktk uchumi wa taifa...kwanza hawakwepi kodi...na hata hivyo ni kama wanakuwa na double taxation pale wanapopokea mishahara yao...na pale wanapo enda kununua bidhaa...wakibanwa hawa hata mfanya biashara hapumui
 
Mkuu wafanyakaz wa serikali ndio nguzo kuu ktk uchumi wa taifa...kwanza hawakwepi kodi...na hata hivyo ni kama wanakuwa na double taxation pale wanapopokea mishahara yao...na pale wanapo enda kununua bidhaa...wakibanwa hawa hata mfanya biashara hapumui
Ivi Tanzania inawafanyakazi wangapi wa umma na wanagap wa sekta binafsi , tuanzie hapo kwanza.
 
Back
Top Bottom