Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Hatua ya serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plasitiki kumetoa fursa kwa wajasiriamali jijini Arusha kushiriki mafunzo ya muda mfupi ili kupata elimu ya kutengeneza Mifuko mbadala ya Makaratasi kwa ajili ya vifungashio.
Wakiongea katika hafla ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili ya kutengeneza vifungashio kwa kutumia Karatasi ,katika chuo cha Ufundi cha Tanganyika Polytechnic, baadhi ya wahitimu hao wameishukuru serikali kwa kupiga marufuku matumizi ya Mifuko ya plasitiki kwani imewawezesha kupata fursa ya kujifunza kuzalisha Mifuko mbadala itakayowawezesha kujiajiri na kuongeza kipato.
Wakiongea kwa niaba ya wenzao wahitimu hao,Martha Mwakidebe,Rose Chisala na Neema Mgendi wameipongeza serikali kwa hatua ya kuzuia matumizi ya Mifuko ya Plasitiki kwakuwa wao kama wajasiriamali wadogo imewapa fursa ya kujifunza na kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kuzalisha Mifuko mbadala.
Meneja wa shirika la viwanda vidogo SIDO,Nina Nchimbi ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo,aliwataka wahitimu kutumia fursa hiyo kuanzisha viwanda vidogo kwa ajili ya kuzalisha vifungashio kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono Sera ya serikali kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Amekipongeza chuo hicho cha Tanganyika Polytechnic kwa ubunifu na kuanzisha mafunzo ya ufundi stadi,yatakayowasaidia kujengea uwezo wa kufanyakazi za kuzalisha kupitia ujuzi walioupata.
Awali Mbunifu wa Mitaala katika chuo Hicho Dkt Richard Masika,Alisema nia ya chuo cha Tanganyika Polytechnic ni kujenga uwezo wa ujuzi kwa wajasiriamali ili wawe na uthubutu wa kuanzisha viwanda vidogo na kuondoa dhana iliyojengeka kwamba wenye uwezo wa kuanzisha viwanda ni wageni kutoka nje ya nchi.
Alisema mbali na chuo hicho kutoa mafunzo ya ujasiriamali ,kinatoa mafunzo ya ufundi wa Tehama,Umeme wa jua na umeme wa Majumbani pamoja na Udereva na kuwataka jamii kuwa na tabia ya kujiendeleza ili kupata ujuzi utakaosaidia kuanzisha viwanda vidogo.