Wajane . . . . . !!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Kwenye jamii yetu kuna tabia inanikera sana,tena sana.
'
Tabia hii ipo hasa kwetu wanaume.
'
Unakuta ndugu yako wa kiume amefariki na ameacha mjane na watoto na Mungu alikua amemjaalia mali na fedha kwenye akaunt za kutosha
'
Na wakati anahangaika na mkewe kutafuta mali na fedha hizo nyie ndugu mlikua huko mnakokujua nyie wala hata kuja kumsalimia ndugu yenu hakuna,mnajidai mko busy,leo mnasikia kafariki mnakuja kudai usimamizi wa mali!
'
Hivi mlikua wapi?
'
Ndugu yenu alipokua anahangaika na mkewe mlikua mnafanya nini?
'
Mnamsababisha Mjane wa ndugu yenu apate msiba mwingine wa usumbufu wenu wanaume wazima na famili mnazo mnatoa macho mali ziliztafutwa na mwanaume kama nyie?Hii ni aibu!
'
Leo ndo wanajidai eti wanawapenda watoto wa marehemu,nyambafu!!
'
Napata wazo la kuweka mwongozo wa kale ka kiwanja kangu ili nikija kuoa mke wangu asisumbuliwe!
 
Tunaambiwa kila siku tuandike wosia lakini tunaona kama ni kujichulia hivi; acheni wake za wadogo zetu au wa kaka zenu na nephews/nieces zenu wale mali zenu badala ya wake zenu na watoto zenu!
 
Eiyer nakubaliana na wewe. Ni vizuri kuweka ka muongozo mapema kama una ujasiri wa kufanya hivyo. Muongozo ni msaada mkubwa sana kwa akina dada wanaopata matatizo ya kupoteza waume zao wa ndoa na hasa pale ndg wanapota kujimilikisha mali za marehemu na kumuacha mjane na watoto hawana pa kukimbilia.
 
Tunaambiwa kila siku tuandike wosia lakini tunaona kama ni kujichulia hivi; acheni wake za wadogo zetu au wa kaka zenu na nephews/nieces zenu wale mali zenu badala ya wake zenu na watoto zenu!

Haiwezekani!Lazima nikurithishe aisee!
 

Mali zangu mwenyewe nikose ujasiri wa kuziamulia?Haiwezekani!Labda sio mimi!
 
Mali zangu mwenyewe nikose ujasiri wa kuziamulia?Haiwezekani!Labda sio mimi!

Wengine huwa wanaogopa wanafikiri kuandika urithi ni kujichulia kifo, hujawahi kusikia mambo haya mdogo wangu? :A S angel:
 
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh smell fishy
 
Heri yako umelitambua mapema, maana huwa tunaishi kwa kujifunza makosa ya wengine.
 
Baba akifiwa na mkewe anaitwaje?
 
Hii tabia ni ubinafsi na uroho wa mali ufanywao na baadhi ya wanafamilia.
Ila sababu kubwa isababishayo udhia huu, ni ile fursa aipatayo mwanamke ya kuolewa tena na mwanaume mwingine.
 
Ukikua utajua . . . . .!!
Hahah...mbona unatoa majibu ya rejareja hivyo??
Suala la kujua au kutojua maana ya nadharia yako sidhani kama linahusiana na ukuaji au rika. Ukweli ni kwamba huwezi ainisha madaraja ya "uoga" kulingana na rika la mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…