Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
WAJA HATUNA HIYARI.
1
Nyayo hufuata ndia, Maliki alo ipanga,
Mja huwezi kimbia, chungu yake pakanga,
Huna hila kufikia, asali kwenye mzinga,
Hakika Mola hupanga, kila kitu hujalia.
2
Sijaribu kudhania, mwenyewe waweza panga,
Hebu kwanza zingatia, jahazi na lake tanga,
Upepo hufuatia, labda ishushwe nanga,
Hakika Mola hupanga, kila kitu hajalia.
3
Mwenda mbio hana njia, angakazana kuwanga,
Afanye kukusudia, akupatie majanga,
Mola takupigania, midhali hakuyapanga.
Hakika Mola hupanga, kila kitu hujalia.
4
Kwa nguvu ukajitia, huko na huku kutanga,
Kuti kujitafutia, kwa mashekhe na waganga,
Ka hajakuandikia, jua utayabananga,
Hakika Mola hupanga, kila kitu hujalia.
5
Mchele wajipatia, kwa kuutwanga mpunga,
Kama ukiyapatia, si ujuzi wa kulenga,
Allah kakujalia, kiumbe wata kuringa,
Hakika Mola hupanga, kila kitu hujalia.
6
Hapa kikomo natia, sasa nawata kulonga,
Nilo sema zingatia, kiumbe yatakujenga,
Mwisho naomba Jalia, atukinge na majanga,
Hakika Mola hupanga, kila kitu hujalia.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Whatspp/call 0622845394 Morogoro.