Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Mbunge wa jimbo la Ukonga Mheshimiwa Mwita Waitara amesema bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linapitia kipindi kigumu mno na linahitaji maombi kuliko hata Rais JPM.
Akiongea na vijana wa CHADEMA wa Chuo kikuu cha Dodoma katika mkutano wao wa ndani wa chama katika kijiji cha Ng'ong'ona uliohudhuriwa pia na Mbunge Anatrophia Theonest na viongozi wengine wa BAVICHA na BAWACHA, Mh. Waitara amesema mkakati uliopo ni kulifanya bunge kuwa chombo cha kupiga mhuri maamuzi ya serikali chombo kisichohoji chochote. Ametolewa mfano tabia inayoendelea ya kuwalazimisha wabunge wa ccm kukubali kila kitu na kuwapangia nini cha kuzungumza.
"..Wabunge wa ccm wanadaftari lao kila mtu anaandika amechangia nini.."
Mh. Waitara amesema wabunge wa ccm wanaochangia tofauti wanapigiwa simu na ikulu na kutishwa, akiwataja baadhi ya wabunge waliopokea simu za vitisho kutoka kwa Magufuli kutokana na michango yao, amemtaja Mh Marry Nagu na Mh Lusinde.
Pia Mh Waitara alipata nafasi ya kuzungumzia vyuo vikuu ambapo amedai kuwa amepokea data mbalimbali za ufisadi kutoka chuo kikuu cha CBE, ufisadi wa zaidi ya milioni mia nne. Aidha amesema kuna mfanyakazi wa CBE ambaye yupo jela lakini amepandishwa cheo na anaendelea kulipwa mshahara mnono ambao hauonekani unaenda wapi! Amemuomba Mh Rais katika utumbuaji wake awamulike CBE na alipatie bunge uhuru wake limsaidie kutumbua majipu.