katika pitapita hapa jf nikakutana na uzi unalalamikia kutozwa kwa channel za ndani yaani local channels wakati bunge lilipitisha kuwa local chanels zionyweshwe bure... sasa bwana mkubwa yule (mtoa post kule) alikuwa anasikia tu wenzake wakilalamika na kwa mujibu wa yeye mwenyewe alikuwa anaona watu wanalalamikia kitu kisichokuwapo kisa yeye nyumbani kwake anaangalia local channels bila malipo. Alisahau kuwa wakati bado haujafika kwa king'amuzi chake kulipia local channels...ilipofikia zamu yake haraka haraka akaibuka una uzi huo wa kulalamikia wizara ya habari utamaduni na michezo( sina hakika kama ndio wizara inayohusika kulishughulikia hili)
Ninachitaka kuwakumbusha watu hapa jf ni kuwa tusijisahau sana, hawa wapinzani ndio midomo yetu sasa waache waseme na wala tusiwadharau maana itafika wakati hiki wanachokilalamikia kitafika kwako. je utamlalamikia nani na wewe unaona watu eti wanatafuta umaarufu....kweli??!!...ukipenda kitu penda kwa kiasi maana hayo ni maumbo na kwa hiyo yanabadilika.
ahsanteni...
Punda tausikia mlio wake.