Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
MWITA Waitara, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam amesema, marufuku ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara nchini inatokana na kukosekana kwa fikra pevu miongoni mwa viongozi,anaandika Regina Mkonde.
Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Uongozi Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam amesema hayo leo katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi’ kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Star TV.
“Anachofanya Rais Magufuli ni kuzuia siasa za Chadema ili tusijiimarishe huku yeye akisuka mipango ya CCM kusikika peke yake pia anadhibiti vyombo vya habari vinavyoandika ukweli, hii ni siasa ya kitoto,” amesema na kuongeza;
“Maamuzi yaliyofanyika si ya haki, Magufuli amezuia mikutano ya Chadema anaruhusu ya CCM tu, mwanzo alikataza mikutano ya hadhara lakini alipoona chama chake kitahitaji kufanya mikutano akaruhusu wabunge kufanya kwenye maeneo yao, jambo hili si sawa.”
Waitara amesema kuwa inashangaza kuona hata tamko la kuwataka wabunge na madiwani peke yao kufanya siasa katika Kata na Majimbo yao likikiukwa kwa kuwaruhusu viongozi wakuu wa CCM kufanya mikutano lakini viongozi wa upinzani wakizuiliwa.
“Christopher Ole Sendeka ni msemaji wa CCM na siyo Mbunge, amefanya mkutano mkoani Arusha na polisi walimlinda wala hawakumzuia, lakini ukiacha hilo vyama visivyo na wabunge au madiwani vitajijenga vipi na kupata wabunge wapya bila mikutano?” Amehoji.
Katika hatua nyingine, Waitara amesisitiza adhima ya Chadema kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu ili kupinga viashiria vya udikteta ambavyo vimeanza kuonekana katika serikali ya awamu ya tano.
“Kufanya mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na kisheria kwa vyama vyote vya siasa, na UKUTA upo pale pale kwasababu hii ni nchi ya vyama vingi, kama Chadema hatufanyi mikutano ya maendeleo watuache, waitishe ya kwao na watushitaki kwa wananchi,” amesema.
Magufuli kawavuruga, kila mtu anataka kujipima ubavu.Watu kwa kusafiria nyota.!!!!!
Wewe uko nchi gani?Naomba kuuliza hii nchi inaongozwa kwa katiba au amri...??
Wanajipima ubavu, wanadhani itawasaidia kuwashawishi wananchi wawaone wanaweza Waitara tunamwangalia tu huku UKONGA, 2020 bila kitu tunambwaga hainaga USHEMEJI hiyo.Naona imekuwa wakati muafaka kwa kila kila mbunge wa chadema kupata kick kwa kutumia jina la magufuli.
Hakuna cha maana alichokisema, ni mwendelezo ule ule wa kutafuta umaarufu. Aliyoyasema yamesemwa sana na watafuta umaarufu kama yeye, wamemuwahi.Mhe Waitara kaongea hoja za msingi.
Lakini sitashangaa kusikia leo hii au kesho Waitara kama ilivyokuwa kwa Mhe. Lissu na yeye anatafutwa na Kamanda Ciro kwa uchochezi! Nashindwa kupata lugha ya kuzungumzia huu utawala wa John Pombe Magufuli na PM wake Majaliwa Majaliwa! Ni timu mbovu kabisa ambayo haijawahi tokea hapa Tz!
Nasikia hawa jamaa wote ni Waalimu na Waalimu huwa wana sifa moja ya kwamba ni WAELEWA. Lakini hii pair naona ni kinyume chake! Yawezekana ni wale Waalimu walioingia enzi zile kwa utaratibu wa UPE(Ualimu Pasipo Elimu)! Hawa walikuwa ni waalimu waliotokana na kufeli Darasa la 7 kuingizwa kwenye Ualimu.
Pengine kuna haja ya kuchunguza vyeti vyao!
Ukiwa unashirikisha ubongo huwezi andika hayo uliyoandikaNaona imekuwa wakati muafaka kwa kila kila mbunge wa chadema kupata kick kwa kutumia jina la magufuli.
Mtu akiongea ukweli nikutafuta umarufu sikuhizi kumbeHakuna cha maana alichokisema, ni mwendelezo ule ule wa kutafuta umaarufu. Aliyoyasema yamesemwa sana na watafuta umaarufu kama yeye, wamemuwahi.
Ningekuwa Magufuli ningewapiga stop hata kwenye media maana sasa kero wamezihamiashia huko, kila siku kwenye TV, full kuuza sura.kiujumla mbunge wa ukonga kazungumza ukweli mtupu. waachwe wananchi waamue siku ya maamuzi. kila chama kina haki ya kufanya mikutano na wananchi.
Aisee ni shida!!!!!!Magufuli kawavuruga, kila mtu anataka kujipima ubavu.
Inategemeana ameongea nini, jipya gani alilolisema Waitara ambalo wachovu wenzake hawajalisema?Mtu akiongea ukweli nikutafuta umarufu sikuhizi kumbe