Waislamu wahimizwa kuchangia maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu wahimizwa kuchangia maendeleo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Nov 21, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [h=2]WAISLAMU nchini wametakiwa kujitokeza na kuunga mkono uchangiaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo hususan elimu, ili kujikwamua na lindi la umaskini. [/h]

  Wito huo ulitolewa juzi na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, na mdhamini wa CCM Kata ya Mbagala, Aisha Sururu, katika harambee ya uchangiaji wa Kituo cha Asw-habulkahfi Islamic iliyofanyika huko Yombo Davis Corner jijini Dar es Salaam.

  Harambee hiyo iliandaliwa baada ya madrasa hiyo ambayo hivi sasa inafanya shughuli zake Kariakoo kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi huko Yombo ambako kwa jana zilichangwa sh 375,000.

  Akizungumza baada ya harambee hiyo, Mtemvu aliwasihi Waislam wengine kuzidi kukichangia Asw-habulkahfi Islamic Centre, kwani kitawawezesha kuwa karibu zaidi na hivyo kusaidia katika jukumu la kuiletea maendeleo jamii.

  Mtemvu pia katika harambee hiyo, aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Temeke kuwa ahadi yake ya ujenzi wa barabara si kiini macho, kwani ameishaanza kuitekeleza kwa vitendo tofauti na baadhi ya watu walivyoanza kupotosha ukweli.

  “Ndugu zangu Wanatemeke nawahakikishia ahadi yangu ni ya kweli na utendaji umeishaanza na bado; tunaendelea kuboresha na kujenga barabara, hivyo nawaomba muwe na subira wakati huu wa utekelezaji,” alisema Mtemvu.

  Mbunge huyo alibainisha kuwa, tayari zimepatikana sh bilioni 3 na utaratibu wa kuwapata makandarasi unaendelea kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka Jet hadi Tandika.

  Kwa upande wake, Aisha Sururu, katika kusaidia ujenzi huo ufanikiwe, ameanzisha vikundi vya uchumi kwa kinamama, ili wajiwezeshe kiuchumi hivyo kujiletea maendeleo. Alisema Uislam unazidi kudidimia kutokana na Waislamu kujitenga na kukosa elimu, hivyo aliwataka kinamama kubadilika na kuungana na vijana wao katika kujiletea maendeleo.

  Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
   
 2. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  da waislamu yaani wamechangia tsh 375000 tu kwa ujenzi wa kituo. Lakini nampongeza mbunge kwa kuwahimiza wawe wanachangia maendeleo wenzao walkristo wanajenga shule kwenye harambee wamechangia tsh milion 240+
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Yaaani pamoja na Mbunge Mtemvu kwenda wametoa laki 375,000/- kweli safari bado ni ndefu sana sana ya kufikia ukombozi wa kweli wa elimu kwa upande huo
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawkutaka kualika mafisadi na hela zao chafu. Bora hicho kidogo cha halali kuliko fedha yenye damu na dhambi za kumwaga.
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Something is better than nothing
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wivu wa nini? Nyinyi ni wagumu wa kuchangia, pamoja na huyo Mtemvu kuwepo bado hata lakini 4 haikufika?
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sawa. Unaweza kuita ubahili lakini ni heri shilingi kumi iliyotolewa na muuza mchicha aliyeipata kihalali kuliko wale watakasa fedha na hasa kwa nia ya kujijengea mazingira ya kutwaa madaraka.
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu Wanatemeke nawahakikishia ahadi yangu ni ya kweli na utendaji umeishaanza na bado; tunaendelea kuboresha na kujenga barabara, hivyo nawaomba muwe na subira wakati huu wa utekelezaji," alisema Mtemvu.


  Mbunge huyo alibainisha kuwa, tayari zimepatikana sh bilioni 3 na utaratibu wa kuwapata makandarasi unaendelea kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka Jet hadi Tandika.


  Hizi fedha ni za serekali [walipa kodi au Mtemvu katoa mfukoni mwake]
   
Loading...