Waislamu, Maaskofu waungana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu, Maaskofu waungana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nonda, Jan 10, 2011.

 1. N

  Nonda JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Waitaka serikali kuingilia haraka kurejesha amani
  [​IMG] Mbeya, Iringa wachangia fedha majeruhi waliolazwa
  [​IMG] Maandamano mengine ya Chadema yazuiwa Songea


  Viongozi wa dini ya Kiislamu wameungana na wenzao wa Kikristo kulaani mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi jijini Arusha wiki iliyopita na kuwajeruhi wengine kadhaa.
  Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, viongozi hao wa Kiislamu wa Mkoa wa Arusha walisema wanalaani mauaji hayo na kuitaka serikali kuhakikisha inawachukulia hatua haraka waliosababisha mauaji hayo.

  Imamu wa Msikiti Mkuu wa Arusha, Mohamed Said, alisema hatua hiyo itasaidia kuepusha baadhi ya watu wasio na nia nzuri kuitumia nafasi hiyo kuendelea kupandikiza chuki.
  Imamu Said aliwaambia wanahabari katika mkutano huo uliofanyika kwenye ofisi za msikiti huo kuwa viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuelewa kuwa migogoro yao inayaathiri makundi mengine ya watu wasio wanasiasa.

  Alisema wanasiasa wanapaswa kutambua kuwa amani iliyopo ikitoweka na wao hawatasalimika.

  Source. IPPMEDIA
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  this news lacks clarity!
   
 3. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Kama ungesikiliza vizuri ungejua waislamu wamesemaje. kimsingi wana laani chadema kwa vurugu zilizotokea. pia leo wametoa msimamo wao kuhusu meya wa arusha. wao wamesema kwamba wanamtambua meya huyo na watashirikiana naye kwa hali yoyote katika kazi zake, tofauti na makanisa ambayo yamesema haya mtambui. PIa waislamu hao wa arusha wamesema kuwa wametoa msimamo huo ingawa wanamini kuwa kiongozi yeyote wa kisiasa awe rais, waziri au meya hahitaji kutambuliwa au kukubaliwa na dhehebu lolote. lakini imebidi watoe msimamo wao kwa vile makanisa yamesema hayamtambui wala hayatampa ushirikiano.
   
Loading...