Waifu kajanjaruka!!!

Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
3,391
Reaction score
1,546
wadau,mi waifu wangu sio mtu wa mitandao kabisa japokuwa ni graduate na ana kazi yake.hata acc fb hana,anapenda vitu simpo simpo sana kasoro kuvaa ndo anapenda avae vizuri.amekuwa akiniona mi nashinda na laptop muda wote nachat napost etc etc.ana access na acc yangu ya fb so huwa anaingia kushangaa shangaa.jana jioni kanishangaza sana,amekurupuka tu anaanza kuniambia anataka username yangu na password nayotumia jamii forums.sasa nashangaa waifu kawaje au nani kamjanjatusha hadi akurupuke tu eti anataka acc yangu ya jf
 

Haujatuambia alivokwambia umpe ulimjibu nini?!! Unaweza kumpa tu, kwani kuna lolote la ajabu jf? yeye anaingiaga? JF kwani kuna kutongozana jamani, kama kashajiridhisha na fb kuwa hauna tatizo basi huku jf mbona anakuja kujiridhisha tu pia! Lakini usisahau na wewe kumwomba username yake ya JF, akisema hana muulize ye jf kaijuaje?!! Skutii presha, lakini inawezekana ana mshkaji mwingine pembeni amabaye anamfunza yote haya... HUENDA UNAIBIWA MPWA!
 
Sumpe tu atumie ili na yeye ajue kinachoendelea huku atoke kwenye ujima kwani ukimpa utapungukiwa nini sumfungulie mpya halafu mkabidhi tu
 

nachohofia ni yeye kuona post zangu ambazo zingine hapaswi kuziona
 
mbona ni memba hapa skunyingi
 
anasaka maumivu


vitu vingine watakiwa uviache km vilivyo ukivichokonoa utakoma mwenyewe
me kwa ukweli huwa sipendi karaha na simu ya mtu wala kudai password ya email au fb
staki kuupa moyo wangu ugonjwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…