Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,187
Aliyewahi kuwa Katibu wa Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa mtu akiwa amenyooka kama rula ndani ya CCM, akimaanisha kuwa mtu wa kufuata maadili na taratibu, basi ni vigumu sana kutoboa (kufanikiwa) ndani ya chama hicho.
Polepole alisema hiyo ni kwa sababu kuna watu ndani ya chama, ambao yeye aliwaita wahuni, watakufanyia kila mizengwe ili usifanikiwe kwa sababu wanajua ukifanikiwa utazuia mipango yao miovu ndani ya chama.
Polepole si tena kiongozi wa CCM lakini maneno haya aliyoyasema zamani yamejidhihirisha katika kipindi hiki cha mchakato wa uteuzi wa wagombea udiwani, ubunge na uwakilishi ndani ya chama hicho.
Watu wa ndani ya CCM wakiwamo watia nia na wapambe wao hivi sasa wamalala,ikiana wakituhumiana kwa uhuni katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani.
Wanazungumza kwa siri lakini wote malalamiko yao yanafafa – wahuni wameivamia CCM na sasa wenye haki wamepigwa dafrau.
Uhuni huo unajidhihirisha kupitia vitendo kadhaa kama vitendo vya upendeleo, rushwa iliyokithiri miongoni mwa wajumbe wa kamati za siasa za wilaya na mikoa na matumizi ya vitisho kwa baadhi ya watia nia.
Kuna maamuzi yanafanywa ndani ya chama kutokana na ushawishi kutoka kwa baadhi ya wagombea. Kama si rushwa basi kuna vitisho – wengine wanatishiwa maisha na hivyo kulazimika kufanya uamuzi ambao hauendani kabisa na sifa za badhi ya wagiombea,” alisema mmoja watoa habari wetu.
Angalia kwa mfano katika jimbo la Kilwa Kaskazini. Suala la rushwa, vitisho na ukiukwaji wa taratibu umekuwa mkubwa jimboni humo katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM.
Watu wengi kutoka ndani ya CCM wilayani KIlwa wanasema kuna watia nia ambao hawakuonmyesha hofu yoyote kwa kutoa rushwa. Waliitoa mchana na usiku, bila kificho wala woga.
MwanaCCM mmoja wa jimbo la Kilwa Kaskazini
anasema kuna wagombea watatu katika jimbo hilo ambao kwa kiasi kikubwa wameuvuruga mchakato huo wa uchaguzi kiasi kuwa CCM inaelekea kupata mgombea asiye na sifa zinazostahili.
“Watatu hawa (anawataja majina ambayo siwezi kuyaandika kwa hatua za sasa) wamekwenda kwenye kamati za siasa za kata na wilaya na kugawa fedha kwa mashindano. Hawakuishia hapo, wameikamata si tu kamati ya siasa ya wilaya ya Kilwa, bali pia ya Mkoa. Wamezikamata kwa namna ambayo hizi kamati zimeshindwa kuwa huru kabisa,”
Yeye ana hofu kuwa kwa jinsi mchakato huo ulivyoendeshwa, kuna hatari ya kupata wagombea ambao hawatasaidia sana katika jitihada za serikali kuwaletea maendeleo wananchi.
Anasema inasikitisha kuwa licha ya watu hao kufanya vitendo vya rushwa wazi wazi lakini kamati hizo za siasa au kamati za maadili hazikukemea vitendo hivyo.
Anasema ilifikia hatua watu hao, kila mkoja akawa anatamba hadharani kuwa jina lake lisiporudi viongozi wa kamati hizo wanakosa pa kuweka sura zao huku mwingine akisema fedha waliyokula wajumbe wa kamati hizo imeziweka roho zao rehani.
Mtoa habari huyo anasema maneno hayo yalisemwa na mmoja wa watia nia ambaye anajulikana kwa tabia zake za kutembea na silaha na kuwatishia watu anaokosana nao hata katika masuala madogo madogo.
“Upo uwezekano kuwa kamati hizi zimeandika taarifa na kuzipeleka ngazi za juu. Ni muhimu sana taarifa hizo zikazingatiwa kwa sababu haya mambo yametokea kweli na yanakitia chama doa kubwa.”
Anasema kwa mazingira hayo upo uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati za siasa walifanya maamuzi kwa hofu ili kuepusha shari dhidi yao.
Alisema inashangaza sana mchakato ambao ulipaswa kuwa wa siri taarifa zake zimevuja mitaani ambako kila mtu anajua ni akina nani ambao majina yao yamependekezwa na kamati hizo.
“Hali hii inatia mashaka iwapo kamati hizi za siasa zimefanya kazi zake sawasawa. Majina ya walioteuliwa yanapaswa kutangazwa na Kamati Kuu lakini hivi sasa huku mitaani watu wameshaanza kampeni wakiamini kuwa majina yao yamepitishwa.”
Kuhusu ukiukwaji wa taratibu, anasema kuwa Chama kiliweka utaratibu mzuri sana lakini kilichofanyika ni kinyume kabisa na utaratibu uliowekwa na chama.
Mathalani, watia nia hawakutakiwa kwenda majimboni kabla ya muda. Lakini wengi wamekiuka sharti hili. Watu wemekwenda na watu waliokwenda ni watu wenye fedha nyingi.
Anasema wengine walikwenda kwa kisingizio kuwa huko ni kwao lakini walikuwa wanafanya kampeni jambo ambalo halikuruhusiwa.
“Nimeamua kuongea nawe kwa sababu naamini waandishi wa habari na vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuwezesha mabadiliko. Tunaomba mtusaidie katika hili. Kuna ambao watadhani kuwa ninazungumza haya kwa ajili ya siasa, hapana, lengo langu ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata wawakilishi bora katika vyombo vya kufanya maamuzi,” anasema.
Hali ni mbaya maeneo mengi.
Mtia mwingine kutoka jimbo lililoko kanda ya Ziwa Viktoria alisema kuwa yale matangazo kutoka kwa viongozi wa juu wa CCM kuwa suala la rushwa halitavumilia katika uchaguzi huu ni kama yaliingia kwenye sikio moja na kutokea sikio jingine.
“Yaani huku rushwa ni wazi wazi. Wala hauwezi kuamini kuwa hili ndilo jambo ambalo lilikemewa na viongozi wetu wa juu kwa ukali kabla ya kuanza kwa mchakato.”
Mtia nia huyo anaonekana kuwa amekata tamaa kutokana na yeye kutotumia fedha kuwahonga wajumbe.
“Hali huku kwetu si nzuri, kifupi inakatisha tamaa kabisa, rushwa iko nje nje. Binafsi sitarajii kama jina langu litapita kilichobaki ni kudra za Mungu pekee, tuombeane.”