Wahujumu uchumi nao ni mafisadi tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahujumu uchumi nao ni mafisadi tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kandambilimbili, Apr 26, 2009.

 1. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #1
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa tutafika tu
   
  Last edited: Apr 26, 2009
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna haja ya kuelewa na kulinganisha dhana kama uhujumu uchumi, kudaiwa, ufisadi, wizi, kuteka dola nyara, kukwepa kodi na kadhalika.

  Kudaiwa siyo kosa mbele ya sheria au jamii. Kwa kawaida wafanyabiashara, na hasa biashara endelevu huambatana na kudai kwa upande mmoja na kudaiwa kwa upande mwingine. Biashara isiyokuwa na component ya wadai na wadaiwa huo ni ubangaizaji ambapo shughuli nzima utegemea pesa ya mfukoni ya mfanyabiashara husika. Vinginevyo pesa ya uwekezaji katika biashara (mercantile) huenda sambamba na huduma za mabenki. Na hapa kuan haja ya kuelewa kuwa kutoa mikopo ndiyo shughuli mama/mahsusi ua mabenki yote duniani. Hivyo, kwa upande mmoja, mabenki lazima yadai au kudaiwa na wateja wake.
  Vitendo vyote vya kifisadi, kuteka dola nyara, wizi wa mali ya umma, kukwepa kulipa kodi na kadhalika, ni vitendo vya kuhujumu uchumi. Kwa hiyo mafisadi na wakwepa kodi wote ni wahujumu wa uchumi. Ila wadeni wa mabenki siyo wahujumu wa uchumi. Chukua mfano huu hapa. hadi sasa Tanzania inadaiwa dola billion 15 za kimarekani. Wadai wa Tanzania ni pamoja na Benki ya Dunia. Lakini bado Benki ya Dunia inaendelea kuikopesha Tanzania (hivi majuzi imeipatia stimulus package ya dola million 200), na hivyo hatuwezi kusema kuwa Tanzania inahujumu uchumi wa benki ya Dunia.
  Kama Bwana Reginald A. Mengi alikuwa andaiwa au bado anadaiwa kiasi chochote na mabenki hakiwezi kukubalika kuwa ni kitendo cha kuhujumu uchumi. Hiyo ni shughuli ya kawaida ya katika mercantile world. Kama Mkapa aliuza NBC haikutokana na shinikizo la Bwana Mengi kudaiwa na banki hiyo (maana deni hilo lingeendelea kubaki deni hadi leo), bali ilitokana na shinikizo la Benki ya Dunia na Fuko la Fedha Duniani (IMF), kwa upande mmoja, na ujinga wa Serikali ya Mkapa kwa upande mwingine. Hadi sasa kuna nyaraka zinazoonyesha kuwa Mkapa kupitia kampuni yake ya AnBen alipokea dola 500,000 za kimarekani kutoka ABSA walionunua NBC bila hata kulipa hata senti moja huku wakitetewa na Mkapa. Hakuna nyaraka yoyote inayoonyesha kuwa Bwana Mengi alipata chochote kutokana na kuuzwa NBC bila malipo. Aidha ni muhimu tukafahamu kuwa wakati huo Mkapa alikuwa amekamia kumfilisi Bwana Mengi, na uhusiano wao ulikuwa mbaya.

  Vilevile, ingefaa tukafahamu kuwa watu aina ya akina Azim Dewji ni wabangaizaji vichwani na kimatendo. Hawana hata kanadharia kokote ka kuwasidia kujadili jambo kutokana na uelewa/utambuzi ila kwa kuona, kunusa, kulamba, kugusa au kusikia kitu. Wamekuwa wakifanya biashara za kubangaiza bila mipango yoyote. Kuendelea kuwapo kwao katika biashara ni pale biashara inapoendeshwa kwa mchezo mchafu wa kukwepa kodi au kuhonga (rushwa) watendaji wa serikali. Nakumbuka Dewji alishindwa kuendesha kiwanda chake cha mafuta ya kula (Garage, Mandela road) baada ya kugundulika kuwa alikuwa anakwepa kodi na hivyo kutakiwa alipe kodi! Alikacha! Baadaye kati ya mwaka 1999-2002 alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kukwepa kulipa kodi (katika biashara yake nyingine). Kesi hiyo mpaka leo bado ipo (lakini imekuwa very slow, labda aliishapenyeza rushwa). Huyo ndiye Azim Dewji. Kwa taarifa hii naye ni mhujumu uchumi (laiti angejua maana ya uhujumu uchumi asingetamka maneno hayo).
  Tuache ushabiki wa nani kasema nini. Tulipende taifa letu Tanzania, na tuwe tayari kulikomboa. Tushirikiane na yeyote mwenye nia nzuri na mkakati sahihi wa kuikomboa Tanzania kutoka katika makucha wa mafisadi. Tusikubali kutumiwa na wezi hao.
  Wakhtanabahu
   
 3. 911

  911 Platinum Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Tunazidi kuwatambua kwa rangi zenu.Hivi nikikopa then nikawa sirudishi au nikashindwa kurudisha si kuna procedure za mdai kuzifata ili apate chake???Hizi baseless allegations ni za wale ambao juu ya shingo zao wamebeba TOFALI.
  Hivi hamuoni aibu mnapoandika huu ududu??I wish mngekuwa exposed kuliko hivi sasa mnapojificha nyuma ya pc maana ndipo mnapopata courage ya kuandika utumboutumbo.Mwaka huu hatuwaachi,keko ni yenu.
   
Loading...