SuperEnthusiasis
Member
- Feb 4, 2023
- 39
- 75
Habarini wa JF,
Wazazi na ndugu wa karibu huenda walijitahidi kwa hali na mali na kujibangaiza kwa kidogo walichopata ili watoto wasome, na kweli watoto hawa walijitahidi kusoma kwa bidii mpaka kufikia ngazi za juu za elimu. ambapo kwa nchi yetu level yenye wasomi wengi zaidi ni Degree/bachelor.
kadri miaka inavyozidi kwenda ndio idadi ya wahitimu inaongezeka na graph ya wahitimu wa vyuo inapanda., mbaya zaidi watoto hawa wanahitimu huku wengi wao wakiwa hawajui waelekee wapi. na ukizingatia karibu 80% ya watoto hawa wametoka kaya masikini kiasi kwamba familia zao zinawatazama kwamba sasa huenda wakazikomboa familia zao.
Uwezekano wa kupata ajira ni mdogo, uwezekano wa kuweza kukidhi mahitaji yao wenyewe tu unaweza kuwa ni changamoto. nani awasaidie watoto hawa?.
Watoto hawa wanahitaji msaada wa kisaikolojia ili watulize akili wanapoingia mtaani, pia watoto hawa wanahitaji connections za michongo ili wajikwamue kiuchumi.
Wengi wao wamejawa na stress juu ya hatua gani wachukue kwa sasa wakiwa wanaelekea kumaliza mitihani yao ya mwisho. wengi wanajiuliza je warudi nyumbani kwao mikoani au wabaki kwenye miji ambayo wamesoma chuo waanze mihangaiko hapo?, wapo dilemma.
Na sio kweli kwamba watoto hawa hawataki kazi ngumu au biashara ndogondogo kisa wana elimu kubwa, la hasha.
Binafsi pia namaliza chuo kikuu mwaka huu,. degree ya mechanical engineering. nilianzisha kibiashara ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwenye kunipatia mahitaji na hata uhakika wa kula na kulala. lakini biashara hii siyo mwisho wa malengo yangu, nahitaji fursa ya kunyanyuka na kuanza maisha mapya yenye muelekeo ulio thabiti.
Kiukweli wengi wa wahitimu huwa kazi walizozisomea hawazijui, na mimi nikiwemo, ili niwe engineer kamili ninahitaji muda wa kujifunza kwa kupitia internship na wengi mnajua hili. kama kuna nafasi ya internship sehemu basi nitashukuru sana nikipata.
Pia, sio lazima internship au kazi niliyosomea, hata kama kuna wazo ambalo sokoni linalipa kwa sasa naomba utuandikie hapa ili wengi tufaidike,. pia ushauri nao sio mbaya.
Mbarikiwe na iwe jumapili njema kwenu.