KERO Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIUT) 2025 hatujapewa vyeti mpaka leo

KERO Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIUT) 2025 hatujapewa vyeti mpaka leo

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba tusaidiwe wanachuo tuliomaliza Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto toka mwezi wa saba mwaka jana mpaka leo tarehe 28.01.2026 hatujapewa vyeti kwa course tulizomaliza. Tumekuwa tukipigwa danadana tuu na huu pasipo kupewa vyeti vyetu.

Tunapishana na nafasi za ajira sambamba na fursa za kuomba kujiendeleza kwa ngazi ya juu ya elimu kwa dirisha la mwaka jana mwezi wa 11 na sasa dirisha la mwezi wa tatu na wanne lakini kama haitoshi ni kushindwa kufanya recategorisation kwa wale waliopo makazini

Nimeambatanisha na ujumbe wa Makamu wa Rais wa Serikali kuja kwa wanachuo na bado imekuwa ni siasa

---------
TAARIFA MUHIMU KWA GRADUATED STUDENTS
Kwenda Kwa Wanafunzi Wote Waliograduate

Zoezi La Kupritiwa Vyeti Litaendelea Tareh 26/01/2026 Na Kutakuwa Na Utaratibu Ufuatao

1. Vyeti Ambavyo Vitaprintiwa Na Kusainiwa Wahusika Watakuwa Notified Kupitia Simu Zao Za Mkononi
2. Transicripts Na Vyeti Vitatolewa Kwa Utaratibu Wa Mawasiliano Kama Ujapijiwa Simu Au Kupokea Sms Tafadhali Subiri Mpaka Utakapopokea Ujumbe Kuonesha Vyeti Vyako Vipo Tayar
3. Kwa Ambao Hawajafanya Clearence Endeleeni Kufanya Clearence Ili Vyeti Vyeti Vipritiwe On Time Kama Procedure Zinavyoeleza

N.b Office Ya AR inasisitiza Kama Ujatumiwa Ujumbe Au Kupewa Taarifa Tafadhali Usifike Chuoni Mpaka Utakapojulishwa Ili Kuepusha Msongamano Usio Na Ulazima,Tafadhali Zingatia Taarifa Hii Na Kufata Maelekezo


Guild Vice President KIUTSO
SALUM A.MAROBOTA
0656078258
 
Ada wanataka ila vyeti wamegoma kutoa
 
Kiu wako after Ada.
Hayo mambo mengine hayawahusu.
Wahitimu mngejiorganize mwende na waandishi wa habari mkinukishe.
Siku hiyo hiyo mngepewa vyeti venu.
Shida ya watz ni uchawa na uoga kila sehemu
 
Back
Top Bottom