Ili kuzielewa methali, misemo na nahau hizi za wahenga inabidi kwanza kujua muktadha halisi na mazingira katika nyanja zote za maisha yao wakati walipozitunga. Na nyingine maana yake halisi huwa imejificha sana mpaka uchimbue kwa ndani.
Na kwa vile jamii hubadilika badilika, methali, misemo na nahau hizi nazo inabidi zibadilike kuendana na mabadiliko ya jamii husika. Hata misemo na nahau zenu za sasa vijana, huko mbele ya safari pengine zitaonekana hazina maana yo yote kulingana na maisha halisi ya wakati huo.
Tafuta wazee wa Kiswahili wakueleze maana halisi ya hiyo methali "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni" na ilitumika katika mazingira gani. Utashangaa sana!