Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,273
- 25,297
Akizungumza katika mahafali ya 19 ya Chuo cha Uhasibu Arusha, wakati akitunuku vyeti vya ngazi na kozi mbalimbali kwa wahitimu 1,324 mwishoni mwa wiki.
Dk. Kijaji alisema baadhi ya wataalamu wa uhasibu wanachangia kurudisha nyuma maendeleo kwa tamaa zao.Alisema ni vema watumie elimu waliopata kubuni ajira na pale watakapotoa wafanye kwa weledi na uadilifu.
"Mjue mkiwa na tamaa ya kutajirika haraka kwa kutumia vibaya fedha za umma mnasababisha kukithiri kwa umaskini miongoni mwa jamii ya Watanzania, kwa kuwa asilimia kubwa mmechangia kurudisha nyuma maendeleo kwa baadhi yenu," alisema.
Alisema endapo wataalamu hao watabadilika na kuwa na uadilifu itawezesha taifa kufanikisha ndoto yake ya kufikia uchumi wa viwanda kabla ya mwaka 2025.
Aidha, alipongeza chuo hicho kuwa wabunifu wa kuongeza kozi kulingana na mahitaji ya jamii hadi kufikia 33 ikiwamo ya shahada mpya ya kijeshi ilioanza kutolewa mwaka huu.
Kuhusu ombi la ujenzi wa hosteli na kumbi za mihadhara, alisema serikali itazitatua kulingana na jinsi inavyopata fedha, japo alishauri uongozi wa chuo kuhakikisha wanazishirikisha sekta binafsi.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, Dk. Faraji Kasidi, alisema mwaka huu wameadhimisha mahafali ya 19 ya chuo hicho na ya nane kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Coventry cha Uingereza.
Aliishukuru serikali kwa kutoa mikopo kwa nusu ya wanachuo wa mwaka wa kwanza 2017 na kufanikisha ndoto kwa watoto wanaotoka familia maskini.
"Lakini nawasihi wahitimu mkafanye kazi halali ili mpate vipato halali badala ya kutafuta utajiri wa haraka," alisema.
Chanzo: Nipashe