Watanzania watalia usiku na mchana wakisema wana Maisha magumu, watasema wanataka mabadiliko. Lakini Kikwazo kikubwa ni Wahariri nchini kuishi bila kujitegemea kimawazo, bila kuweka maslahi ya taaluma zao mbele, wao hubaki kujikomba kwa Mashirika makubwa nchini yawafadhili pesa kwa ajili ya vikao, Pindi Mashirika hayo yanapopatwa na kashfa mbalimbali hayaandikiki sio kwa sababu yana kasoro ila aibu ya kuwaandika wale wanaowafadhili. Watanzania ambao sio wahariri angalieni habari za mashirika kama NSSF, LAPF, PSPF zinavyoandikwa. Chunguzeni habari za Matajiri na wafanyabiashara kama Mengi, Manji, Gulam Dewji,na wamiliki wadogo wa vyombo vya habari wanaotembeza bahasha kwa wahariri na kuhonga Wabunge kama anavyofanya Alex Msama anayetuhumiwa kufanya uvamizi katika viwanja vingi Dar. Wahariri wanahangaishwa na Mwanasiasa kijana wanasumbua taifa kwenye mijadala isiyo na tija, sasa 25 Octoba hayupo nchini anawaandikia habari na kuwatumia kuwa anaalikwa Ulaya, bado mnakimbizana kuwapelekea Watanzania mambo mepesi kama hilo. Taifa litaangamia, Wahariri wa Tanzania tabia ya kutumika mtaacha lini ili wananchi waandikiwe habari za ukweli kwa maendeleo ya nchi? Gazeti moja limeandika Ufisadi kuhusu Ufisadi wa Tanescho na Mwanasiasa mmoja anavyolifilisi kwa ushauri wa kisheria, tayari wahariri kadhaa wameshakimbilia kwa Mwanasiasa huyo Mwanasheria kuacha kulishambulia gazeti lililoandika Ufisadi wa Tanesco........ Tanzania nakupenda kwa Moyo..............................