Wahanga wa mafuriko Dar wapatiwa eneo mbadala!!

Pindima

JF-Expert Member
Aug 16, 2011
347
81
Uongozi wa Mkoa wa Dar es
Salaam tayari umeandaa eneo la
ekari 200 lenye viwanja 2,800
katika eneo la Mbopo, wilaya ya
Kinondoni kwa ajili ya wote
walipoteza makazi yao kutokana
na mvua kali na mafuriko katika
jiji la Dar es Salaam.
 
Uongozi wa Mkoa wa Dar es
Salaam tayari umeandaa eneo la
ekari 200 lenye viwanja 2,800
katika eneo la Mbopo, wilaya ya
Kinondoni kwa ajili ya wote
walipoteza makazi yao kutokana
na mvua kali na mafuriko katika
jiji la Dar es Salaam.

tatizo la nchi hii ni kuwa sheria zipo lakini haziheshimiwi, kwa kiwango kikubwa tumekuwa tukiwalaumu wananchi wadogo wadogo kwa kujenga mabondeni....mvua za juzi zimetudhihirishia kuwa si hao walalahoi tu amabo ni vulnerable bali hata taasisi za kuheshimika mfano KAJIMA pale jangwani....hivi ni nani aliwapa ruhusa kajima kujenga bondeni kama vile, au yule tajiri aliyezungusha ukuta pale kigogo sambusa?

hata baada ya hatua hii ya kutoa viwanja, mara baada ya maafa haya kupita, watu watasahau na kuendelea na maisha yao kama kawaida na ni muhali kuona watu wenye vibanda vyao walivyovijenga kawa kujinyima sana wakihama na kwenda huko makazi mapya.....pengine mfano kwanza uwe kwa matajiri....KAJIMA, Yule wa kigogo sambusa na mwingine yupo pale TABATA matumbi kulia kama unatoka ubungo kwenda Buguruni.
 
Sawa sawa uyasemayo al zagawi hii ni nguvu ya soda tu muda ukipita yote hayo yatasahaulika!
 
Wangewajengea kabisaa kwenye hivyo viwanja kwa mikopo nafuu ya serikali. Unafikiri watapa wapi hela za kujengea wakati hata vitanda vyao vimesombwa na maji?
 
jeshi la kujenga taifa wawezeshwe ili wajenge hapo nyumba za mtindo mmoja na kwa muda mfupi.
Najua wanaweza sema wanazarauliwa.
 
Kwa ufisadi wa bongo Hata hvyo viwanja hao wahanga hawatavipata,mafisadi wa ardhi ndio watagawiwa
 
mi nadhani kama hilo litatekelezwa basi serikali inapaswa kupewa hongera...kuna mengi inavurunda lakini katika uamuzi huu naipa big up na hongera sana...tu napata shaka kama hivi viwanja vitawafikia walengwa maana kuna watu wapo tayari wanasubiri kujinufaisha kupitia mgongo wa hawa waathirika...so hilo liangaliwe kwa umakini zaidi
 
Back
Top Bottom