X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,120
Awali ya yote napenda sana kuwapongeza vijana wa Tanzania kwa moyo wa Uzalendo na Uvumilivu mkubwa tulio nao. kwakweli nikiwa muhanga wa kusubiri ajira Serikalini kama tulivyozoea, kutokana na viongozi tunaowategemea kushindwa au kwa makusudi hawatoi matamko yanayoeleweka, hivyo kupelekea vijana wengi kupoteza uelekeo maana mtu anawaza anaweza kuanzisha kilimo cha mboga mboga mara ajira zimetoka bustani atamuachia nani? Hivyo napendekeza tukiwa kama vijana tunaoitakia mema Nchi yetu ni bora tukatumia njia halali ya MAANDAMANO kuishinikiza Serikali itoe tamko rasmi kuhusu Ajira, nadhani wote tunajua kuwa Ajira ni ugonjwa wa UKOMA ulioshindikana Dunia nzima hivyo tuiombe serikali isiogope kutoa tamko lolote kwani sio Tanzania tu pekee ndio yenye uhaba wa Ajira.
KUHUSU MAANDAMANO HAYO
Maandamano hayo nataka yafuate misingi yote ya Kikatiba kuanzia vibari na ulinzi kutoka kwa Jeshi la Polisi hivyo kabla atujaandamana mimi mwenye nitajitolea kwenda kwa viongozi mbali mbali kuwaomba ushauri kwanza. tutawaomba ushauri ata wanausalama {Polisi} kisha tutaanzisha hayo maandamano.
DHUMUNI LA MAANDAMANO
kama nilivyo andika hapo juu kuwa Maandamano hayo lengo mahususi ni kuishinikiza serikali itoae tamko rasmi kuhusu ajira, maana kumekuwa na mpishano wa maneno kwa baadhi ya viongozi tunaowategemea hivyo watahiniwa tumeshindwa kujua ni kauli ya nani tuifuate, kupitia Maandamano haya naamini serikali itatoa tamko moja.
SEHEMU RASMI YA MAANDAMANO
Kwakuwa Dar-es-salaam ndipo ilipo ikulu napendekeza maandamano haya ya amani tuyafanyie huku huku Dar-es-salaam.
haya ni maoni yangu binafsi napendekeza maoni mengine zaidi ili tupate muafaka mapema.