Wahamiaji Haramu Kutoka Uhabeshi:Uhamiaji Imulikwe

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam Wanajamvi,

Kwa miaka mingi tumekuwa tukishuhudia wimbi la raia kutoka Ethiopia wakikamatwa nchini. Wanakamatwa katika mikoa mbali mbali, Mbeya, Pwani, Morogoro nk.

Jana tarehe 1/5/2017,siku ya Mei Mosi, kituo cha ITV kilionesha kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku, raia hao wa Ethiopia wakigombea mikate baada ya kukaa muda mrefu bila kula.Kabla ya kupewa chakula wengine walionekana kulegea na kulala kwa ajili ya njaa.

Kinachoshangaza ni kuwa wahamiaji hao wanaolenga kwenda Afrika Kusini hukamatwa tu baada ya kutelekezwa na wenyeji wao. Aidha, wahamiaji hao hawakamatwi wakiwa wanavuka mpaka wa Kenya kuingia Tanzania. Hukamatwa wakiwa wamefika katikati ya nchi au wanakaribia kuingia mpaka wa Tanzania na nchi jirani. Hii inaonesha kuwapo genge linalohusika na biashara hii likihusisha uhamiaji na polisi.

Imetokea wengine kuwekwa ndani ya mapipa ili wasionekane au kwenye container. Wengine hukutwa wamekufa kwa kukosa hewa ya kutosha au chakula.Ni wakati mwafaka kuwawajibisha maafisa uhamiaji wa mpakani mwa Tanzania na Kenya kwa kuwa wanahusika.

Huwezi kukamata wahamiaji halafu ukawaacha wasimamizi wa mipaka wanapovuka wahamiaji.Polisi huonesha mbwembwe nyingi wanapowakamata kana kwamba ni hodari sana.
Nawasilisha.
 
Hahahaaa., Hapo kwenye mbwembwe za polisi ni kweli kabisa, huwa wanakuwa na mbwembwe as if walikuwa wanawafuatilia kwa miaka nenda rudi.
 
Back
Top Bottom