Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewakamata wahamiaji haramu wapatao 22 ambao walikua wakisafiri kutoka nchini burundi kupitia kigoma, Tabora kwa basi na kisha kuelekea nchini Zambia wakiwa kwenye usafiri wa basi aina ya AN.
Miongoni mwa wahamiaji hao tisa wakiwa ni watoto wadogo ambao walikua wameambatana na wazazi wao katika safari yao, wamekamatwa wakiwa wanaingia kwenye kituo kikuu cha mabasi mjini Tabora ndani ya basi hilo ambalo linafanya safari zake katika mikoa ya Tabora na Kigoma.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora Mjini John Mfinanga ambaye aliongoza kikosi kazi cha Askari Polisi wasaidizi amesema wamefanikiwa kuwakamata raia hao wa Burundi baada ya kupata taarifa za siri juu ya ujio wa raia hao ambao walikua wakipita mkoani humo wakielekea nchini Zambia.