Wahadhiri kuteuliwa, vyuoni atabaki nani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
wahadhiri.jpg

Kwa miaka mingi wengi walizoea kuona wasomi walio wengi wa taaluma wakibaki kufundisha vyuoni hadi kumaliza utumishi wao.

Hata hivyo, miongoni mwao, wachache walikuwa wanapata fursa adhimu za kiuongozi, hasa wale walioamua kuachana na taaluma na kuwania nafasi za uwakilishi kama ubunge.

Kwa miaka ya karibuni, hasa tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, wasomi wengi wameteuliwa kushika nyadhifa nyingi serikalini, za utendaji, ukurugenzi, uwaziri na sasa za kisiasa, wengi wakitokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Baadhi ya walioteuliwa katika nafasi hizo ni Profesa Paramagamba Kabudi, waziri wa Katiba na Sheria na Profesa Kitila Mkumbo, katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Pia, wamo mkurugenzi wa Tenesco, Gavana Benki Kuu, mwanasheria mkuu wa Serikali na wengineo.

Wiki iliyopita, Watanzania wameshuhudia tena uteuzi mwingine tena, safari hii ni Dk Bashiru Ali aliyetangazwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM kuchukua mikoba ya Abdulahman Kinana.

Uteuzi huo pia umezua mjadala miongoni mwa wasomi, huku baadhi wakiunga mkono na wengine wakihofia kupungua kwa wabobezi vyuoni.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Dk Jimson Sanga anasema pamoja na kuunga mkono uteuzi wa wasomi kwenye nafasi za uongozi, anashauri uteuzi huo ulenge katika uzalishaji zaidi.

Anasema kwa miaka mingi wasomi wamekuwa wakitumika kama viwanda vya kuzalishia watenda kazi, na wao kubaki palepale na kuwa matumaini ya Watanzania ni kuona matokeo makubwa zaidi huko wanakopelekwa.

Dk Sanga anasema itakuwa kazi bure kama wasomi wanaoteuliwa hawatapewa uhuru wa kutosha wa kufanyia kazi yale wanayoyajua kuhusu taaluma walizobobea.

“Kila sehemu sasa hivi wapo maprofesa, madokta na wasomi wengine wengi, hivyo tunatarajia kuona matokeo makubwa zaidi,” anasema na kuongeza;

“Nchi ya India ilivyotaka kuleta mabadiliko na kuwekeza kwenye teknolojia iliajiri wasomi na kweli waliing’arisha nchi yao, natamani kuona hayo yanatokea hapa kwetu.”

Hata hivyo, Dk Sanga anasema kuondoa mtizamo wa kusababisha upungufu vyuoni, teuzi zinazofanya zinapaswa kuwa kwenye vyuo vikuu vyote kwa usawa badala ya kutazamwa kimoja tu.

Naibu Makamu Mkuu wa UDSM-Tafiti, Profesa Cathbert Kimambo anasema wasomi wanao mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi ndio maana katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli kumekuwa na teuzi nyingi zinazowahusu.

Anasema japo teuzi hizo zinaathiri chuo kwa maana ya kupunguza nguvu kazi katika ufundishaji, umuhimu wa kundi hilo kuingia katika masuala ya kiuongozi ni mkubwa kwa kuwa wana uwezo kiutendaji.

“Sisi tunalichukulia kama jambo chanya kwa sababu linakiletea chuo chetu sifa na inaonyesha wanataaluma wetu wana uwezo mkubwa... anaongeza,

“Ukweli ni kwamba inachukua muda kuziba pengo la mbobezi aliyetoka, hata kama tutaajiri wengine bado tunahitaji kuwasomesha na kuhakikisha wanafikia kiwango cha juu zaidi kwa asili ya kuwasaidia wanafunzi,” anasema Profesa Kimambo.

Mtizamo wa Profesa Kimambo hauko mbali na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika chuo hicho, Dk Rasul Ahmed Minja.

Dk Minja anasema japo si rahisi kumtengeneza mhadhiri kwa siku moja, lakini uteuzi huo unaonyesha nao wanao mchango mkubwa kusukuma gurudumu la maendeleo.

Dk Minja anaeleza kuwa wasomi wana mchango mkubwa na wanaweza kusaidia katika kulifikisha taifa kwenye hatua nyingine ya kimaendeleo, hivyo teuzi zao kwenye nyadhifa mbalimbali ni sahihi.

Hata hivyo, anasema teuzi za wasomi vyuoni zinaleta changamoto lakini wanapambana kuhakikisha wanaendelea kutengeneza wengine siku hadi siku.

Mhadhiri mwingine mstaafu na mtaalamu wa saikolojia, Profesa Issa Musoke anasema teuzi za Rais Magufuli zinaonyesha mabadiliko makubwa kisiasa nchini.

Anasema wengi walizoea kuona anateua makada kwa kufahamiana hata kama hawana uwezo wa kuongoza katika nafasi walizopewa.

Profesa Musoke anasema teuzi zinawaangalia hata wasomi ambao hapo nyuma hawakuwa wakifurukuta kwenye ulingo kwa kiuongozi kama ilivyo sasa.

“Tulizoea kuona kada anapewa cheo hata kama hana uwezo au fisadi, uteuzi huu binafsi umenifurahisha sana,” alisema alipozungumzia uteuzi wa Dk Bashiru.



Wanafunzi walalamika

Japo wahadhiri wengi wanaonyesha kufurahi wenzao wanapopata nafasi za kiuongozi kwa kuteuliwa, hali ni tofauti kwa wanafunzi.

Wengi wanaona wameachwa solemba hasa wale waliokuwa wakisimamiwa kwa ukaribu na wasomi.

“Niliposikia jina lake (Dk Bashiru) kuwa ameteuliwa nilipatwa bumbuwazi, kwa kweli sijawahi kujuta kumfahamu mwalimu wangu, nasikitika kwa kuwa anaondoka ila nafurahi kwa sababu amepata nafasi nyingine,” alisema Mwanafunzi wa Uzamili, Palma Kawishi.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisimamiwa na Dk Bashiru anasema anafurahia kwa sababu mwalimu wake ameongeza hatua nyingine kimaisha, lakini pengo lake ni gumu kuliziba hasa kutokana na ubobezi aliokuwa nao.

Mwanafunzi mwingine wa shahada ya kwanza, Josephina Massawe anasema kinachobakia kwao ni bumbuwazi kwa sababu walimu wao wenye ujuzi wanapungua.

“Kwetu wanafunzi uteuzi huu ni changamoto kubwa kwa sababu wasomi wanapungua, hata hivyo tunamuombea heri mwalimu wetu (Badhiru),” alisema.

Mwanafunzi mwingine Nyakunga Faraja anashauri chuo kuendelea kuwapika wahadhiri zaidi ili wanapoteuliwa na kuondoka kwenye nafasi zao kusiwe na upungufu wowote.

Chanzo: Mwananchi
 
Tatizo si ku appoint wasomi. Wasomi ndio wanaotakiwa.

Tatizo ni.

1. Usomi ni nini? Kuwa na Ph.D haitoshi kumfanya mtu msomi. Kama mtu ana Ph.D halafu ni muoga hawezi kumbishia kistaarabu bosi wake, huyo si msomi. Ni mganga njaa. Wasomi wa Tanzania wengi ndio wako hivi.

2. Huko vyuoni wanakotoka, wameandaa watakaokuja kuchukua nafasi zao? Kuna transfer of knowledge process? Kuna transition period? Kuna handover process? Au mtu anateuliwa tu "effective immediately" anakurupuka kutika chuoni mpaka ofisi aliyokuwa aappointed bila handover process?

3. Kuna wasomi wengine wa kutosha kuchukua nafasi zao?
 
Kikubwa ni kwamba wasomi (levoo ya Pi Ech Dii) ni nyenzo adhimu (scarce resource) kwa Tanzania yetu na unaweza kuwatumia kwa majukumu tofauti nje na ndani ya akademia. Kiasilia hii ni nyenzo ya kufanya utafiti na au kufundisha elimu ya juu. Na kwa Tanzania wengi wako vyuo vikuu kama inavyotegemewa na hata huko hawatoshi (angalia staffing list ya vyuo).
Tatizo hili linaendana na ukweli kuwa Tanzania bado ni tegemezi sana sana sana kwenye kuwekeza kwenye nyenzo watu levoo ya masters na phd tunategemea ufadhili wa nnje na hatutumii hela yetu wenyewe ( ukiacha mishahara ya wahadhiri) lakini hakuna scholarship zakuzungumzia (ingawa bodi inasema inatoa mikopo kwa wahadhiri kusomea hizo digirii). Hivyo nje ya pool la vyuo mtu anapochaguliwa na kuhamishiwa serikalini inakuwa vigumu kumpata mbadala wake na hata kuajili katika ngazi ya chini sio rahisi kama wengi tunavyo amini.
Na sasa ameingia mdudu anaitwa LAWSON kule utumishi-huyu amekuja na yake: wale wenye masters kwa kutumia research peke yake wanatupwa nje na mfumo huu, kwani unadai GPA. Lakini hawa kawaida ni vijana ambao wana ufaulu wa juu kwenye degree ya kwanza. LAWSON pia anavigezo ambavyo sio rafiki na grading systems ya ndaki fulani ambazo kwa mfano zinahitaji wanafunzi wawe wamepata marks za juu kupata grade kama ya B au B+. Zamani ndaki hizi zilikuwa zinachukua kwa mfano mwenye B avarage sasa inatakiwa B+ hivyo hupati wahitimu wa kutosha wenye hivyo vigezo. Huku ukimchomoa professa basi ndiyo imetoka kwani kupata T.A pia ni ngoma nzito.
Lakini kama nilivyosema hawa watu duniani kote kazi yao ya msingi ni kufundisha na utafiti-sasa ukipata ugonjwa wa kuamini kwamba ni watendaji wazuri na ndio unaowataka huko serikalini na ukawachomoa kwa style ya mlipuko basi ni wazi taaluma ita athirika. Na ubaya wa taaluma maumivu yake huonekana huko mbele sana ya safari. Mwishowe Kupanga ni kuchagua.
Siku hizi wanasema vyuo vina sucession plans, na hata wanapotoa mikataba wakubwa wanataka wazione hizi succession plans na zipo lakini kama hazipati funding ni sawa na hewa tu.
Mwishowe tukumbuke kila chuo kinataka kuongeza namba ya wanafunzi na hicho ndo kile serikali inachotilia mkazo. Hivyo student to instructor ratio inazidi kuharibika.
Ni vigumu kwa vyuo vya umma kukiri kwani funding yao kubwa inatoka serikalini na serikali ndio inao wachomoa hao wahadhiri lakini kuna idara zina hali ngumu kutokana na hili.
 
alipoteuliwa Dr kadeghe Mika kuwa DC nilipata na B+ ya CL 106 udsm.

acha yateuliwe tu yana roho mbaya sana.
Kama mchango wako uko based kwa hilo uko sawa lakini hapa tunaongelea issue pana zaidi. Kwa hiyo angekuwepo ungepata ngapi mkuu?
 
Kama mchango wako uko based kwa hilo uko sawa lakini hapa tunaongelea issue pana zaidi. Kwa hiyo angekuwepo ungepata ngapi mkuu?
Hata kadege angekuwepo asingepata hata c yule mzeee hafai kabisa anapenda sifa za kukamata watuuu
 
Hata kadege angekuwepo asingepata hata c yule mzeee hafai kabisa anapenda sifa za kukamata watuuu
Sawa, lakini hiyo haihalalishi kuhamisha wahadhiri kutoka vyuoni kwenda serikalini kwa kiwango tunachokiona na elimu isiathirike.
 
Back
Top Bottom