Wagonjwa waanza warejea Muhimbili, KCMC, Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagonjwa waanza warejea Muhimbili, KCMC, Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 15, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Hali ya huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imerejea kuwa katika hali ya kawaida baada ya wagonjwa walioondoka kutokana na mgomo wa madaktari kurejea kupata huduma.
  NIPASHE jana ilishuhudia idadi ya wagonjwa ikiwa imeongezeka huku madaktari na wauguzi wakizunguka katika wodi wakitoa huduma kwa wagonjwa. Afisa Uhusiano Mwandamizi wa hospitali hiyo, Aminieli Eligaesha, alisema kila kitu kinakwenda sawa na idadi ya wagonjwa imeanza kuongezeka.
  Kwa upande wa Taasisi ya Mifupa (MOI) NIPASHE ilishuhudia huduma zikiendelea kama kawaida, na Afisa Uhusiano Msaidizi wa Taasisi hiyo, Frank Matua, alisema wanahudumia wagonjwa kama kawaida. Aliongeza kuwa hata huduma za kliniki zimeanza kutolewa kwa wagonjwa wote.
  Katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, idadi ya wagonjwa imeongezeka hasa wasio wa dharura ambao wamekuwa wakipokelewa kwa wingi.
  Katika hospitali ya Rufani ya KCMC, idadi ya wagonjwa imeoongezeka, baada ya kuihama kutokana na mgomo huo.
  Baadhi ya wgonjwa jana walionekana wakiwa katika foleni wakisubiri kuingia kwa daktari ambapo wengi wao walielezea kuridhishwa kwao na huduma
  wanazozipata na kusema kuwa ni huduma nzuri na bora ukilinganisha na awali.
  Naye mmoja kati wa daktari katika hospitali hiyo, Nkoronko Mugisha alisema hali ya utendaji kazi kwa madaktari hospitalini hapo ni ya
  hali ya juu na wanafanya kazi kwa hari kubwa.

  Idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya imeongezeka na NIPASHE ilishuhudia misululu mirefu ya wagonjwa waliokuwa wakijiandikisha kuonana na maaktari.

  Imeandikwa na Samson Fridolin na Ninaeli Masaki, Dar; Emmanuel Lengwa, Mbeya ma Charles Lyimo, Moshi.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...