Wagonjwa 220 watibiwa Uvimbe, mirija Muhimbili

Wagonjwa 220 watibiwa Uvimbe, mirija Muhimbili

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1550901816343.png


HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imefanikiwa kuwatibu wagonjwa 220 wakiwamo wenye uvimbe wa kinywa kwa kutumia mfumo wa radiolojia tangu kuanzishwa kwa Kitengo Radiolojia hospitalini hapo mwaka 2017.

Mbali na uvimbe kwenye kinywa, watalaamu wa hospitali hiyo pia wamezibua mirija ya nyongo, kuweka mirija kwenye figo ambayo mirija yake imeziba na kunyonya uvimbe wa maji na usaha kwa kutumia utaalamu wa kisasa bila kufanya upasuaji. Mkuu wa Idara ya Radiolojia wa MNH, Dk. Flora Lwakatare, aliyaeleza hayo jana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya matibabu na mafunzo yanayoendelea katika Tawi la Mloganzila, yakitolewa na wataalamu kutoka Marekani.

Alisema kuwa katika kambi hiyo iliyoanza Februari 4, wamefanikiwa kutoa tiba ya uvimbe kwenye matiti kwa wanawake 40 na lengo ni kuwatibu wanawake 50 ifikapo Machi 9, mwaka huu.

“Tunaishukuru serikali kwa juhudi zake za kuhakikisha matibabu yanapatikana nchini, pia kuwezesha kununua vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya huduma za matibabu badala ya kwenda nje ya nchi. Huduma hii imewanufaisha Watanzania wengi na kuokoa fedha nyingi,”

Dk. Flora alibainisha kuwa, kwa wastani mgongwa mmoja mwenye uvimbe anatumia Sh. milioni mbili kupata matibabu, lakini awali walilazimika kutumia Sh. milioni 96 kupata huduma hiyo nje ya nchi. Alisema watalaamu wao wanatumia vifaa kama X-Ray, CT-Scan, Utrasound na kuchukua sampuli kwenye uvimbe kwa kutumia utaalamu wa kupitisha sindano eneo husika badala ya kufanya upasuaji.

Dk. Flora pia alisema wanatibu maeneo ambako ungefanyika upasuaji mkubwa ili kutoa uvimbe, hivyo huduma hiyo kutolewa kisasa na kuepusha mgonjwa kukaa muda mwingi hospitali. “Kwanza, mgonjwa anatumia muda mfupi kupata matibabu, anaweza kufanyiwa siku hiyohiyo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Pia tunatumia vifaa vinavyoweza kubaini kama usaha unaotoka kwenye uvimbe ni dalili ya saratani,” Dk. Flora alisema. Alisema wanashirikiana na wataalamu kutoka vyuo vya Marekani na Austria ambao wapo nchini na vifaa vyao vya kisasa vinavyotumika kufanya uchunguzi na tiba.

Daktari Bingwa Radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yale, Marekani, Dk. Frank Minja, alisema wanapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanafunzi madaktari kutoka Muhimbili ambao wanapata mafunzo hayo. Alisema vifaa vilivyopo nchini vina uwezo wa kufanya matibabu hayo na kilichokuwa kinakosekana ni ujuzi wa wataalamu kutoa huduma hiyo.

“Tumeshirikiana na Muhimbili kutoa mafunzo haya kupitia kambi hii ya matibabu. Tumefarijika kuona katika muda mfupi wa mafunzo madaktari wetu wa mafunzo wameweza kuelewa na kufanya vyema matibabu, hivyo tunaamini tukiondoka wataendelea wenyewe kufanya matibabu,” alisema. Dk. Minja pia alisema wana mpango wa kuanza kurasimisha mafunzo ya radiologia katika vyuo vya nchini ili wanafunzi wapate shahada ya diolojia ya tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.
 
Mwaka huu kila kitu mtaishukuru serikali hata kwa mambo ambayo ni haki yetu walipa kodi😏😏😏😏
 
Back
Top Bottom