Wagombea URAIS WENGINE loh@@@@ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea URAIS WENGINE loh@@@@

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Oct 25, 2010.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  hizi kura jamani embu wagaieni chadema tubadilishe nchi jamani usijelaumu mwenyewe

  Watanzania sasa kupata nafuu ya maisha Send to a friend Monday, 25 October 2010 08:26 0diggsdigg


  [​IMG] Mgombea urais wa UPDP Fahm Dovutwa

  Geofrey Nyang’oro
  MGOMBEA urais wa (UPDP), Fahm Dovutwa amewataka watanzania kufanya mabadiliko makubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kumchagua yeye ili waweze kupata unafuu wa maisha.

  Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Manzese jijini Dar es Dar es Salaam juzi alisema hadi sasa sera za chama chake pekee ni nzuri na kwamba zitakomesha rushwa na uonevu.
  “Sera za UPDP ndizo zenye uwezo wa kukomesha rushwa, uonevu na kufufua usimamizi ambao ndio chanzo cha kumomonyoka kwa msingi wa utaifa hapa nchini,”alisema Dovutwa.

  Dovutwa ambaye mkutano wake huo alihutubia akiwa amekaa kutokana na kuumwa alisema Watazania wanahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika uchaguzi wa mwaka huu ambao umekuwa mgumu kutoakana na aina ya wagombea waliosimamishwa na vyama vyao.

  Alisema sera yake ambayo inasema ardhi kwanza itawawezesha Watanzania kupata maisha bora kwa kuwa watamiliki ardhi badala ya ardhi hiyo kuendelea kumilikiwa na serikali.

  Alisema Serikali ya CCM imewaonea kwa kiasi kikubwa kutokanana kitendo cha kunyang’anya watu ardhi bila ya kuwatafutia maeneo mbadala jambo ambalo limewafanya watu kuishi katika mazingira magumu.
  “Mimi nasema ardhi kwanza kwa sababu ardhi hiyo ilikuwa mikononi mwa wananchi tangu zamani na kutaifishwa na serikali mwaka 1962,huu ndio ubaya mkubwa uliofanywa kwa Watanzania,”alisema Dovutwa.

  Dovutwa alisema kitendo hicho ni uonevu na kusisitiza kama ataingia madarakani kazi za kwanza ni kurudisha ardhi kwa wananchi.

  Katika hatua nyingine Dovutwa alisema serikali yake itawarudisha watawala wa kimila (Watemi) waliokuwepo tangu kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru kwa kuwa watawala hao wakimila waliondolewa kwa hila.

  Dovutwa ambaye amechelewa kuanza kampeni zake kutokana na kuumwa alisema hana shaka juu ya hilo kwa kuwa vyombo vya habari vinaweza kutumika kusambaza habari zake na watu wakamchagua.
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pole na ugonjwa fahmi na karibu kwenye ulingo wa kisiasa
   
 3. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Jitoe tu kwenye hiki kinyanganyiro; too late kusema uchaguliwe
   
Loading...