Wagombea urais nchini Kenya kupambana katika midahalo mitatu mwezi Julai

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,383
3,643
Kamati andalizi inayoshughulikia midahalo ya wagombea urais kupitia runinga na vyombo vingine vya Habari nchini Kenya imetoa ratiba kuhusu midahalo hiyo itakavyofanyika kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti. Itakuwa ni mara ya pili katika siasa za nchi hiyo kwa wagombea wa urais kukutana ana kwa ana katika mdahalo kuweka wazi ajenda zao na kujibu maswali.

Wachira Waruru Mwenyekiti wa Kamati hiyo ametangaza kuwa kutakuwa na midahalo mitatu.
Mdahalo wa kwanza utakuwa kati ya wagombea urais pakee yao utakaofanyika tarehe 10 mwezi Julai kuanzia saa moja na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.

Wagombea wenza nao watakuwa na siku yao tarehe 17 mwezi Julai, huku mdahalo wa tatu na wa mwisho ukiwakutanisha tena wagombea urais tarehe 24 mwezi uo huo wa Julai.

Wakati uo huo, Tume ya Uchaguzi nchini humo imetangaza kuwa wagombea wote wa urais 18 wawasilishe vyeti vyao tarehe 28 mwezi huu.

Wagombea hao ni pamoja na Profesa Michael Wainaina mgombea binafsi, Peter Ondeng -chama cha Restore and Build Kenya Party, Abduba Dida - Tunza Coalition, Kennedy Mongare – chama cha Federal Party of Kenya.

Ekuru Aukot - Thirdway Alliance Party, Joe Nyagah -Mgombea binafsi, Nazlin Omar - Mgombea binafsi, Cyrus Jirongo- UDP, Uhuru Kenyatta - Jubilee , Raila Amolo Odinga ODM kupitia muungano wa NASA.

Wagombea wenine binafsi ni pamoja na: David Munga, Stephen Oweke Oganga,Robert Mukwana Juma,Joseph Ngacha, Japheth Kavinga, Nixon Kukubah,Joseph Musyoka, Erastus Nyamera.

Licha ya wagombea hawa, ushindani mkubwa ni kati ya rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga ambao pia walipambana mwaka 2013.
 
Kwa hali tuliyonayo kisiasa hapa kwetu Tz, mwamko wa kisiasa umeongezeka,wagombea hawatakwepa mdahalo 2020
 
Kwa kweli Kenya huwa tumejiandaa na kuwa wa kwanza Afrika kwa mambo mengi, tatizo wanasiasa wetu hutuangusha, utaona kwenye hii midahalo watakavyoachia misamiati na kuonyesha uelewa wa ndani juu ya suluhu za matatizo ya nchi, lakini utekelezaji zero.
 
Kama hii debate itainvolve more than 2 candidates, it's not worth it.
Hauwezi leta mtu kwa televisheni ambaye ata kwa opinion polls hapati 1%.

Uhuru na Raila wapambane. Hawa wengine wakitaka wapambane kando.
 
Back
Top Bottom