GE2025 Wagombea ubunge wa upinzani Chalinze wahamia CCM

GE2025 Wagombea ubunge wa upinzani Chalinze wahamia CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,233
Reaction score
3,807
Wagombea wawili wa ubunge wa Jimbo la Chalinze, Mkoa wa Pwani, wametangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025

Wagombea hao ni Bw. Waziri Towakali wa Chama cha The United People's Democratic Party (UPDP) na Bw. Kamana Masudi wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), ambao wote walikuwa wakigombea ubunge kupitia vyama vya upinzani jimboni humo

Wote hao wanahania CCM Oktoba 27, 2025, katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Kata ya Bwilingu, Halmashauri ya Chalinze, Mkoa wa Pwani

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Aboubakary Mkawa, aliwakabidhi wanachama hao wapya kadi za uanachama mbele ya umati wa wananchi na wafuasi wa CCM

Mgombea ubunge wa CCM, Ridhiwani Kikwete, ambaye anatetea nafasi hiyo, alishiriki katika tukio hilo na kuwapokea rasmi wajiunge hao wapya

Akizungumza katika mkutano huo wa kuhitimisha kampeni, Ridhiwani Kikwete aliwapongeza wanasiasa hao waliotoka upinzani na kusema uamuzi wao ni ushahidi wa imani kubwa kwa kazi na mafanikio ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya Watanzania


 
Kwa kuwa karatasi za kura zimeishachapishwa na TUME ya uchaguzi haiwezi kuchapisha karatasi nyingine Kwa muda huu mfupi uliobaki. Je. Wananchi wa chalinze wakiwachagua mmoja wa hao waliojiunga na Chama na akapata kura nyingi sana kuzidi yule wa Chama, Tume itafuta Matokeo?
 
umekosea kidogo. Hivyo ni vyama mamluki. Safari hii hakukuwa na hama cha upinxani hata kimoja. Samia hakutaka upinzani. Kwa hiyo uchaguzi umekuwa wa CCM na vyama mamluki yake.
Hii ni mbaya sana Mkuu, tujisahihishe
 
Back
Top Bottom