elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
WAGOMBEA ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo matatu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameainisha vipaumbele vyao katika kuwahudumia wananchi na wameipongeza Kamati Kuu ya CCM kwa kuwapitisha.
Juzi Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM katika kikacho chake chini ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais John Magufuli iliwapitisha wagombea hao, wawili wakiwa wametokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Waliotokea Chadema ni Mwita Waitara anayewania Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam ambalo alikuwa Mbunge wake kabla na Julius Kalanga wa Jimbo la Monduli, Arusha ambaye pia alikuwa Mbunge kwenye jimbo hilo.
Mgombea wa tatu ni Timotheo Mzava aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, anawania Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini lililokuwa chini ya Stephen Ngonyani maarufu ‘Profesa Maji Marefu’ aliyefariki dunia.
Akizungumza na HabariLeo, Kalanga alikitaka Chadema kutojisumbua kusimamisha mgombea kwenye jimbo hilo la Monduli huku akijinadi kuwa atashinda kwa asilimia 100.
Amesema, kwa vile kabla ya kujiunga na Chadema alikuwa CCM, kurejea kwake katika chama hicho kunamfanya kujiona kama simba aliyerejea msituni kwa kuwa anajua mbinu zote za kisiasa za kuwashinda washindani wake kwenye uchaguzi huo.
Alisema, kwa kuwa uamuzi wake wa kurejea CCM umelenga kuwaletea wananchi maendeleo, aliwataka kumuunga mkono ili awatatulie kero zao za muda mefu.
Alivitaja vipaumbele vyake vikubwa viwili kuwa ni kutatua migogoro ya ardhi na kuwatafutia maji wananchi.
Mzava ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kusimamia maendeleo ya kilimo cha chai, ujenzi wa barabara, upatikanaji wa maji na uendelezaji wa mashamba.
Amesema, atawaongoza wananchi hao kwa mbinu mbalimbali kwa kutekeleza majukumu yake ya kibunge huku akisisitiza kushirikiana na wananchi katika kufanikisha hilo.
Mgombea wa Ukonga, Waitara amesema jimbo la Ukonga ni kati ya majimbo ya mjini yanayokabiliwa na changamoto kadhaa za kimaendeleo.
Amesema, kutokana na kuwapo kwake chama cha upinzani, alishindwa kutatua baadhi ya kero na kwa sasa jukumu ambalo CCM imempatia ni kutatua kero hizo na kuleta maendeleo.
"Sikuhamia CCM kwa kununuliwa ila nilivutiwa na sera na mbinu zake za kuleta maendeleo na kwa kuwa wamenipitisha nimejipanga kufanya kweli.”amesema.