Wagombea na ahadi za kuondoa umaskini

Wagombea na ahadi za kuondoa umaskini

Paschalis

Member
Joined
Apr 14, 2012
Posts
41
Reaction score
10
Wana JF
Nimekuwa nafuatilia ahadi zinazotolewa na watia nia ya kugombea urais wa JMT. Karibu wote wanadai kuwa wakipewa ridhaa ya kuingia Ikulu watafuta umaskini kwa Watanzania wakati wa utawala wao. Wengine wanasema wataanzisha au/na watafufua viwanda. Hawajatuambia jinsi gani watahakikisha kuwa viwanda hivyo vitashamiri. Wengine wanasema wataongeza ajira kwa vijana lakini hawajasema jinsi gani watafanya hivyo. Mimi napata mashaka kama kweli wana dhamira ya dhati kufanya hayo yatokee. Hebu angalia umati unaojitokeza kwenda kuwasikiliza na kuwashabikia wakati na muda ambao wangekuwa kazini kuzalisha mali na huduma. Wangapi tunashabikia umati unaojitokeza kuwapokea na kuwashangilia watia nia bila kutafakazi hasara kiasi gani taifa linapata kutokana na masaa ya kazi yanayopotea bure kwa waajiriwa wa sekta rasmi na zisizo rasmi, wakulima na wafanya biashara. La kushangaza wanaotutangazia kuwa wataondoa umaskini wanafurahia umati unaopoteza muda wa uzalishaji kwa kuwashabikia wakijiona kuwa wamefanikiwa, kwangu ni aibu na inanifanya niwe na mashaka juu ya dhamira yao.

Ni wazo binafsi, naomba tujadiliane si kutukanana.
 
Muulize Lowasa watu wa jimbo lake mbona wanapukutika umasikini, porojo tu baada ya kuwasoma watanzania kuwa ni majuha wa kutupwa
 
Back
Top Bottom