Nielewavyo mimi kama mtu mbaya au mshirikina/mchawi atakipata kitovu chako anakuwa na access na wewe. Ni rahisi kwa mwenye kitovu chako kukupata katika anga za kichawi, na kukutumia apendavyo pamoja na kumilikishwa mikoba. Kama hana kitovu itakuwa kazi kwake kukupata kichawi hata kama atakupata. Ndiyo maana katika familia nyingine wakina mama wanaweza kugundua watoto wao ni wachawi wakati hao watoto wameshabobea. Mpaka ugundue kwanza ni kazi. Mimi yalishawahi kunikuta hayo ya kukataa kutoa kitovu cha mwanangu hadi mama Mkwe akamind kama siyo kukusirika. Nimeolewa na mchaga wakati mimi si mchaga, kumbe ukishajifungua tu, mama mkwe (sina uhakika kama ni wachaga wote wanafanya haya) lazima aje kuchukua kitovu, eti wanaenda kuvizika hiko migombani ambako vitovu vyote vya ukoo vinazikwa huko. Cha mtoto wa kwanza nilimpa, na mtoto ikawa bahati mbaya (lakini simaanishi ni kwa sababu ya hiko kitovu nilichompa). Katika kujifunza mambo ya watoto nikajua kuwa kitovu ni kitu sensitive, inabidi nikidestroy mwenyewe kwa kukichoma nk. Nikaamua nikizaa mtoto mwingine wala simpi mtu kitovu bila kujali mila za baba yake. Kilipokatika nikamwambia mume wangu na kumwambia nitakichoma mwenyewe safari hii sitampa mama na sababu nikampa. Mama Mkwe aliposikia hayo alikasirika akaona shughuli yote ya kuja kumuona mwali na mwanaye imekuwa nuksi