Wagombea CHADEMA, CUF wachukua fomu Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea CHADEMA, CUF wachukua fomu Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Aug 28, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  • Dosari iliingia kwa mgombea wa CUF hakuwa na barua ya kuteuliwa na chama chake.
  VYAMA vya Chadema na CUF jana viliuteka mji wa Igunda kufuatia maelfu ya wanachama wa vyama hivyo kujitokeza kuwasindikiza wagombea wao kwenda kuchukua fomu za kuwania ubunge katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi wilayani humo.

  Chadema ndio waliotia fora kutokana na kuwa na msafara mrefu wa magari, pikipiki, bajaji, baiskeli huku watu wengine wakitembea kwa miguu wakiimba nyimbo za kukisifu chama na mgombea wao, Joseph Kashindye.

  Hali hiyo iliwafanya baadhi ya wakazi katika mitaa waliyopita kuacha shughuli zao na kujitokeza barabarani kushuhudia misafara hiyo ya wagombea.

  Kwa upande wa CUF nusura mgombea wake, Lucas Mahona, anyimwe fomu za kugombea baada ya kubainika kuwa hakuwa na vielelezo vinavyoonyesha kuwa chama chake kimemteua kugombea ubunge.


  CUF ndio walikuwa wa kwanza kuingia kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi saa 5:00 asubuhi wakiongozwa na Mratibu wa Uchaguzi wa Chama hicho Jimbo la Igunga, Julius Mtatiro.

  Katika msafara huo wanachama wa chama hicho walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifia mgombea wao muda wote hadi walipofika katika ofisi za Halmashauri ya Igunga ambako ndipo alipo Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.

  Nderemo zao CUF ziliingia dosari msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Protace Magayane, alipogoma kumpa fomu mgombea wao akisema kuwa hana barua ya uteuzi kutoka chama chake.

  "Ni kweli nilikataa kutoa fomu mpaka walete barua ya uteuzi kutoka kwa chama chake na huo ndio utaratibu wa tume," alisema Magayane wakati akieleza juu ya dosari hiyo iliyojitokeza ofisini kwake.

  Hata hivyo, Magayane alisema baada ya kuwapa maelekezo hayo walikwenda kushughulikia na nusu saa baadaye walipeleka barua hiyo na wakafanikiwa kupewa fomu za kugombea na kuondoka eneo hilo.

  Kwa upande wa Chadema hali ilikuwa tete zaidi kufuatia umati mkubwa mara mbili ya ule wa CUF kuingia kwenye ofisi ya msimamizi wakiwa na msururu ya magari, pikipiki, bajaji, baiskeli na huku wengine wakitembea kwa miguu, kumsindikiza mgombea wao.

  Kivutio cha aina yake kilikuwa kwa vijana waliosindikiza mgombea huyo wakiwa wanakimbia, wengine wakiwa wamevua mashati kutokana na jasho, lakini kama hiyo haitoshi, wakati mwingine walikuwa wakisimama na kurukaruka kwa mbwembwe, wakiimba na kupiga kelele za kushangilia.

  Msafara wa Chadema ulifika katika Ofisi ya Msimazi wa Uchaguzi saa 7:00 mchana wakiongozwa na Mratibu wao wa Uchaguzi, Mwikabe Mwita Waitara.

  Msafara huo ulipofika ofisi za Tume ya Uchaguzi ujumbe wa watu wachache uliingia ofisini kwa msimamizi na kuwaacha wapambe wakiwa nje na mara baada ya kukabidhiwa fomu walianza msafara wa kurudi hadi ofisi za chama chao wilayani Igunga.

  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga alisema mpaka sasa wagombea watano wamechukua fomu. Mbali na hao wa Chadema na CUF, wengine ni Said Makeni wa DP, Lazaro Ndageya wa UMD na John Maguma wa SUA.

  Uchaguzi wa Ubunge Igunga unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz, kujiuzulu baada ya kupata shinikizo ndani ya chama chake cha CCM kutaka wanachama wake kujivua gamba.

  Hata hivyo yeye (Rostam) alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kushamiri kwa siasa chafu ndani ya chama hicho, huku akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu Bara, Joohn Chiligati kuwa wamechangia hali hiyo.

  Awali, baada ya CCM kutangaza mkakati wa kukisafisha chama kwa kujivua gamba wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Nnayue na Chiligati walitaja majina ya watu wanaotakiwa kujivua gamba akiwamo, Rostam.

  Katika uchaguzi mdogo wa Igunga, CCM walimteua Peter Kafumu, kukiwakilisha chama hicho baada kushinda katika kura za maoni na anategemewa kuchukua fomu wakati wowote.Kampeni za ubunge katika Jimbo hilo zinatarajiwa kuanza Septemba 7, mwaka huu.
  Source: Mwananchi
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  macho na masikio yako kwenu wana igunga, zidini kutujuza!
   
 3. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chama cha SUA ndio chama gani tena? Hata hvyo mwanzo mzuri kwa Chadema!
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  CDM hapo ni rahisi saana kulibeba jimbo, kinachotakiwa wapenzi hasa vijana wa wakereketwa wa Chadema kulinda kura zao siku ya uchaguzi. Cuf mpaka wameshaprove failure, CCM ndio kabisa Rostam alishaimaliza baada ya kusema kuna siasa za majitaka.
  CHADEMA kanyanga twende.
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Nawashaur wana Igunga wajijotekeze kwa wing siku ya kupga kura. Wasiishie ktk kushangilia.
  CCM wote magamba, hauwez kutoa gamba uweke gamba.
   
 6. m

  matawi JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Kuna utaratibu maganda waliuleta wa kuchangia chama kwa sms wakiuleta chadema nitafurahi sana maana nilitaka pesa ya kampeni isiwe kikwazo. Mtaalamu wa uchumi chadema hebu ifanyie kazi hiyo
   
 7. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ndio kwanza trela picha halijaanza hata kidogo
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kikao gani kilikaa na kwa ajenda zipi je kolumu ilitimia au waliokotana mitaani ili waandike hiyo barua, it seems these people are not seriuos.
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  SUA kilianzishwa na CCM kikiwa na lengo la kushirikishwa uchaguzi wowote Zanz na Bara endapo vyama makini vitasusia.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Vumbi lake wakati wa kampeni ni balaa!
   
 11. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Yote kwa yote pamoja na mbwembwe zooote,wahakikishe daftari la wapiga kura linakuwa updated na kuhakikiwa mapema.Wananchi wapewe fursa ya kuhakiki uwepo wa majina na taarifa zao mapema,makosa ya wakati wa uchaguzi mwaka jana yasijirudie!
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Picha jamani kama kuna mwana jf anazo
   
 13. MANGI MASTA

  MANGI MASTA Senior Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mwandishi wa MWANANCHI mbona kama vile ni kada wa CHADEMA mbona umati wa chadema na ule wa CUF havikutofautina ila kwa chadema waendesha pikipiki walipewa 1000-5000 kila bodaboda baada ya kuona wanawatu wachache mbona hayo hakusema?waandishi wa nmna hii kazi ipo.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  nawe una boda boda au vipi mkuu!
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kwanini CUF na CDM wote wanatumia waratibu wakurya? au Igunga kuna wakurya wengi sana! Nina wasiwasi sana na hii nchni inapoelekea maana kama mtu anasoma hadi kuwa Dr na kuwa mkurugenzi katika ofisi za Umma lakini anarudi kugombe Ubunge, wakati hata huko alipo hakuna alichofanya
   
 16. R

  Radi Member

  #16
  Aug 28, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Usituwekee pumba zako hapa tupewe hela ya nini?Si tunataka mabadiliko hapa,
  tumechoka na maisha,,Nyambafu wewe"
   
 17. p

  propagandist Member

  #17
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umati wa cuf ulikuwa mkubwa wanaotembea kwa miguu chadema waliwakodi boda boda. kwa kweli mgombea wa cuf anapendwa tuache ushabiki.
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  MANGI MASTA,
  Unachosema ni kweli kabisa
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Magamba bado hawajachukua fomu wanasoma upepo bado?
   
 20. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bravo cdm..chama kitakacholeta mafanikio Tanzania
   
Loading...