Wagombea CHADEMA chini ya ulinzi.

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
NI KUDHIBITI RUSHWA, MMOJA AENGULIWA
KATIKA UCHAGUZI
Godfrey Nyang’oro
UCHAGUZI wa viongozi wa Baraza la Vijana la
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), jana ulitawaliwa na vituko
vilivyoambatana na wagombea wa nafasi ya
mwenyekiti, kuwekwa chini ya ulinzi mkali,
ili kuwadhibiti wasitoe rushwa kwa wapiga
kura. Vituko hivyo vilitokea katiKa mkutano
huo wa uchaguzi ulioanza saa 6:00 mchana,
katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es
Salaam na kuendelea hadi usiku.
Katika uchaguzi huo, wagombea tisa wa
nafasi ya mwenyekiti, walitolewa nje ya
ukumbi wa mkutano na kuwekwa chini ya
ulinzi wa mkali wa mabaunsa
wawili.Kitendo hicho kilifanyika wakati
wagombea hao, wakisubiri kuitwa kwa
mahojiano yaliyokuwa yakifanywa na
viongozi wa chama.
Chini ya ulinzi huo, wagombea
hawakuruhusiwa kwenda mahali na hata
pale walipoitwa kwa mahojiano,
walisindikizwa hadi mlangoni.
Mapema uongozi wa Chadema ulipiga
marufuku, wagombea wote kufanya
kampeni nje ya ukumbi wa uchaguzi.
Uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Bavicha
unafanyika baada ya kushindikana kwa
uchaguzi wa awali wa Septemba mwaka
juzi, kufuatia vurugu kubwa zilizosababisha
uongozi kuusimamisha.
Vurugu hizo zilimlazimisha aliyekuwa
msimamizi wa uchaguzi,Charles Mwera
kushindwa kutangaza matokeo na hatua
hiyo ilikuja baada ya kubainika kuwa upigaji
kura, ulikuwa batili.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya kura
zilizohesabiwa kuoenekana kuwa zilizidi
idadi ya waliopiga kura hizo na hakukuwa
na mgombea mmoja aliyepata zaidi ya
asilimia 50 ya kura.
Uchaguzi huo uliwapambanisha wagombea
wengi, lakini waliokuwa wapinzani wa
karibu ni aliyekuwa Ofisa Habari wa
Chadema, David Kafulila na aliyekuwa Diwani
wa Tarime Mjini, John Heche.Wagombea
wengine walikuwa ni Ofisa wa Mafunzo, Day
Igogo na Julieti Rushuli.
Uchaguzi huo wa jana uliwashirikisha
wagombea wa nafasi za wajumbe wa
Baraza Kuu la Vijana na Mkutano Mkuu wa
Taifa wa Chadema.Hata hivyo, akizungumza
kabla ya uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa
chama hicho, Dk Wilibrod Slaa, alisema
baadhi ya majina ya wagombea yamekatwa
kwa sababu ya kutoa rushwa kwa wapiga
kura.
Dk Slaa alisema kuna ushahidi kwamba
mmoja wa mgombea aliyeondolewa, alitoa
rushwa kwa wapiga kura kutoka mikoani
kwa kuwatumia fedha kwa njia ya M-pesa.
Alisema chama hicho kimejipanga kuepuka
vitendo vya ukiukaji wa maadili ikiwa ni
pamoja na kutoa na kupokea rushwa.
"Tulikubaliana ndani ya kamati kuwa
kampeni zote zitapigwa ndani ya ukumbi
wa mkutano,"alisema Slaa. Alisema ni vyema
kila mgombea afuate taratibu zilizokuwa na
chama, ili kufanya uchaguzi uwe utulivu na
wa heshima, hatua ambayo alisema
itakijengea chama sifa.
Mkakati wa kuwadhibiti wagombea
uliendelea hadi Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika alipotangaza taratibu za kuanza kwa
kampeni, ambapo wagombea wote
waliamriwa kutoka nje ya ukumbi na
kuruhusu mgombea mmoja mmoja kwa ajili
ya kujieleza.
Waliokuwa wakigombea nafasi ya
mwenyekiti ni na Aidan Sadick, Benard Mao,
Benard Saanane, Deogratias Kisandu, Edwin
Soko, Grayson Nyakarundu, John Heche,
Masood Suleimani na Mtela Mwampamba.
Nafasi zingine zinazogombewa ni ya
Makamu mwenyekiti bara, Makamu
mwenyekiti visiwani, katibu mkuu, naibu
katibu mkuu, na uratibu na
uhamasishaji.Hatua hiyo ya Chadema
kudhibiti rushwa inakuja wakati mwasisi
wa chama hicho, Edwin Mtei, akiwataka
viongozi wasiwapitishe wagombea
mamluki, kushika nyadhifa ndani ya chama
hicho.
Mtei ambaye alitoa wito huo juzi, alisema
Kamati kuu ya chama hicho, ilitakiwa kuwa
ya kwanza kuchuja majina ya wagombea.
Hadi tunakwenda mtamboni uchaguzi huo
ulikuwa ukiendelea.
Kutohudhuria mahakamni
Akizungumzia sababu za kutokuhudhuria
mahakamani juzi, Dk Slaa alisema ni
makubaliano yaliyofikiwa baina yao na
mahakama kuhusu kutokwenda mara kwa
mara hadi hapo afya ya mmoja wa
washitakiwa, itakapotengamaa.
"Nasikitika kuwa limetokea hili, lakini wote
wanajua sisi ni viongozi wa watu
wasioweza kutoroka. Jumatatu (kesho)
mimi nitakwenda Arusha
kuwasikiliza,"alisema Slaa.
Dk Slaa alisema tukio la juzi lilitokea baada
ya kesi hiyo kutajwa saa 2:00 asubuhi
badala ya saa 3:00 asubuhi.
Alisema kutokana na sababu hiyo wakili
alikwenda mahakamani na kushughulikia
kesi nyingine na alipokwenda kwenye kesi
yao saa 3:00 asubuhi alikuta ikiwa
imeshaahirishwa.
Kuhusu wabunge, alisema kwa sasa
wametawanyika na wana majukumu ya
kitaifa na kwamba hawatakwenda
mahakamani Arusha."Mahakama imetoa
amri ya mimi na wabunge kukamatwa, hata
hivyo ni vigumu kuwapata wabunge wangu,
mwenyekiti wangu atakuwa bungeni
kupokea taarifa ya waziri mkuu,"alisema Dk
Slaa .


SOURCE: MWANANCHI.
 
Back
Top Bottom