Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Niliwahi kusema huwezi kutenganisha uhalifu wanaofanyiwa wafuasi wa vyama vya upinzani na mkono wa wafuasi wa CCM. Mauaji ya kamanda Mawazo, Diwani wetu wa USA River Mhe.Msafiri Mbwambo) aliyeuawa kwa kukatwa kichwa, na viongozi wengine. Nyuma ya mauaji haya kuna mkono wa wafuasi wa CCM. Hata watuhumiwa wa kesi hizi ni wanachama wa CCM.
Ndani ya CCM kuna wagigisi wa mauaji. Wanateka, wanapiga, wanajeruhi na wakiweza kuua wanaua. Kwanini siasa zitufikishe hapa? kwanini siasa zitujengee uadui kiasi hiki?
Siasa ni sera, ni falsafa, ni dira na taswira juu ya maendleo ya nchi. Kama wewe unaamini ujamaa ndio utakaoleta maendeleo katika nchi, na mimi naamini tofauti kwanini unichukie? kwanini upange kunidhuru? Kwanini ukasirike?
Siasa za Afrika ni za ajabu sana. Eti mtu anakuchukia kwa sababu unakosoa serikali inayoongozwa na chama chake. Anashindwa kuelewa kuwa wapinzani hatukosoi kwa nia mbaya bali kuleta changamoto na kufanya serikali iwajibike zaidi. Ni wazi bila upinzani imara serikali itayumba.
Upinzani hutoa dira, taswira, mipango, malengo na vipaumbele vya taifa kama backup kwa serikali. Ndio maana chama tawala kikiona sera nzuri za upinzani huzichukua na kuzitekeleza. Mhe.Edward Lowassa alikiri kuwa sera ya ujenzi wa chuo kikuu Dodoma aliichukua kutoka CHADEMA. CCM hawakuwa na mpango huo. Lakini waliposoma ilani ya CHADEMA (2005 - 2010) waliona ni nzuri na inawafaa, wakaitekeleza. Leo hii maelfu ya watanzania wanagraduate UDOM kumbe ni matunda ya ilani ya CHADEMA. Hizi ndio siasa zenye tija.
Wote tunaijenga Tanzania kwanini tuchukiane? Lengo letu ni kuona Nchi inasonga mbele. Binafsi naamini CCM imeshindwa kutumia rasilimali tulizonazo kufanya taifa hili lisogee mbele kimaendeleo. Sisemi kuwa CCM haijafanya kitu, bali nasema waliyofanya hayaendani na rasilimali tulizonazo. Kiwango walichofanya kwa miaka zaidi ya 55 tangu Uhuru sio ilivyopaswa kuwa. Tulitakiwa kuwa mbali zaidi ya hapa. Huo ndio msimamo wangu na hakuna wa kunibadilisha.
Sasa wewe kama unaamini tofauti jenga hoja kunishawishi. Sio kutishana, wala sio kupanga mikakati ya kufanyiana ubaya. Huo ni ujinga wa kiwango cha PhD.
Nayasema haya kwa sababu kuna kikundi cha vijana wa CCM kinajiita "WAHAFIDHINA" kinapanga kunidhuru eti kisa nakosoa sana serikali yao. Nakosoa viongozi wao. Wamesema "wataninyamazisha". Sasa sijui wanataka kuninyamazishaje. Kama Kamanda Mawazo au? mi sielewi.!
Mmoja wa member wa kundi hilo aitwae "Mutalemwa" anasikitika eti kwanini "wanakufa watu wazima halafu Malisa anabaki".. Seriously?? Kwahiyo anataka kuniua.?
Cha ajabu ni kwamba group hili wapo viongozi wa CCM kitaifa, wapo Wabunge na Mawaziri wanaotokana na CCM lakini hawajaonesha hata nia ya kukemea huu upuuzi. Wanasubiri niuawe kisha watoe "Pole za kinafiki"
Mimi si member wa hilo kundi lakini nina watu humo wanaonitakia mema ambao wamenitumia hizi screenshot zinazoonesha mipango yao miovu. Zipo nyingi but nimeweka hizi chache hapa kama sample ili Watanzania muelewe aina ya vijana wa CCM na akili zao na ili nisivuruge ushahidi.
Tayari nimesharipoti suala hili Polisi na wahusika wanafuatiliwa. Nitatoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha tunakomesha aina hii ya siasa za kishetani. Siasa za kuwaza kuua wengine kisa umepingana nao mawazo. Siasa za kutishana, siasa za kupanga kuumizana.
Pia napenda kuwahakikishia vijana hawa dhaifu wa CCM kuwa hamuwezi kunidhuru kwa vyovyote vile (hata kwa uchawi). MUNGU wangu ni mkubwa sana na ananilinda na watu waovu kama nyie. Mungu aliyenifahamu kabla ya kuwepo misingi ya Ulimwengu aliahidi hataacha mguu wangu uanguke wala kidole changu kijikwae.
Yeye akiwa upande wangu ni nani aliye juu yangu? Yeye aliye nuru yangu na wokovu wangu, nitamhofia nani? Shetani mwenyewe simhofii sembuse nyie vijana dhaifu wa CCM? Biblia inasema "watesi wako wanapokukaribia wataajikwaa na kuanguka mbele zako". (Zaburi 107:28-30, Zaburi 119:105 na Zaburi 27). Kama hamuamini jaribuni muone.
NOTE: Sijawahi kuogopa mwanadamua na sintokaa niogope mwanadamu. Mbinu zenu za kishetani zitashindwa na nimeomba Polisi wawashughulikie ipasavyo ili iwe fundisho kwa vijana wengine wahuni kama nyie.
Malisa GJ.!