Wageni Ndiyo Tutakaoukomboa Mkoa Wa Dodoma

Wageni Ndiyo Tutakaoukomboa Mkoa Wa Dodoma

The Worshiper

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
302
Reaction score
89
Asilimia kubwa ya wakazi wenyeji wa mkoa wa Dodoma wanakaa vijijini,maeneo ambayo yamegubikwa na umasikini wa kutisha wa kimazingira na watu wenyewe.Ni maeneo ambayo hayana huduma muhimu za msingi za mwanadamu,mfano huduma za Maji , Afya, Miundombinu, barabara nk.Ndiyo mkoa unaosifika kwakujaza ombaomba karibu kila mitaa ya miji mbalimbali nchini (hicho ni kiashirio cha umasikini uliotopea na kutokombolewa kifikra).Baadhi ya makabila(wenyeji) ya mji huu ni Wagogo (hapa tulitambue kama kabila kuu),Warangi,wengine ni wanyambwa nk.


Mfumo wa elimu kuchelewa pamoja na huduma nyingine za msingi kwa wananchi zimeufanya mkoa huu uwe na wenyeji wasomi na wawakilishi wachache serikalini wasio majasiri.Viongozi hawa wachache waliopata nafasi za juu za uongozi na uwakilishi wa wananchi wamekuwa hawana lolote la maana wanalolifanya hasa katika kuwasaidia wenzao kufunguka na kuwakomboa kifikra na mtazamo, kutetea,kupigania na kuleta chachu ya mabadiliko na mapinduzi ya kimaendeleo hapa Dodoma.


Wengi wao(viongozi) ni waoga katika kupaza sauti zao ,si wajasiri kukemea,kuihoji serikali juu ya mipango mingi iliyododa na kulala katika mji huu pia karibu wote wanawekeza na makazi yao yapo Dar Es Salaam.Mbaya zaidi na cha kushangaza viongozi kutoka maeneo mengine ndiyo wamekuwa wakipaza sauti zao bungeni kuhusu kero zilizopo hapa Dodoma.


CCM imeshika hatamu Dodoma na kwa kutumia ujinga wa walio wengi wamekuwa wakiendeleza mfumo wa kuwapata viongozi kwa Ukabila.Kwa tatizo hili lililopo la kimfumo na kiutawala hapa Dodoma ni ngumu sana kuwapata viongozi majasiri na wenye nia thabiti (tofauti na makabila haya) kuuendeleza mkoa huu.Katika hali kama hii kamwe maendeleo hayawezi kuletwa na wenyeji kwakuwa wengi wao bado hawajakombolewa kifikra na mtazamo.Naamini Sisi wageni ndiyo tutakaoubadilisha na kuukomboa mji huu wa Dodoma.
 
Umeukomboa mkoa wako kwanza?ebu niambie mkoa gani tz umesalimika na umaskini hali ya tz inafanana kwa kiwango kikubwa ebu nionyesh mkoa gani tz hauna shida ya maji,afya,elimu etc wote tuko kwenye struggle mojatutafute ukombozi kwa tz nzima
 
Dj mbowe amemuandaa dogo mmoja kutoka kaskazini anaitwa alex mushi mwaka 2015 agombee ubunge lengo lao kila mkoa kuwe na wagombea wachagga
 
Tuambie wewe umetoka mkoa gani ambao hauna shida.Mijitu mingine bana inajiona inajuaa kumbe matango tuu
 
Dj mbowe amemuandaa dogo mmoja kutoka kaskazini anaitwa alex mushi mwaka 2015 agombee ubunge lengo lao kila mkoa kuwe na wagombea wachagga

Akiri za kukopi toka kwa magamba wakubwa mpaka magamba vijidagaa hazitofautiani uelewa!
 
Mchaga kuwa kiongoni wa nchi ni ndoto.hata cdm ilipanda tu pale mgombea akiwa si mchaga mmliona hili.
 
Acha pumba, mkoa unaotoka una nini cha kujivunia. Think before you lip!
 
Kwa nini? Na majority ya kabila gani ndio nuru ya taifa.
Makabila nuru yanajulikana ..lengo si kujadili ukabila hapa ila ni kutoa changamoto kwa jamii husika kujikomboa na kushiriki fursa wanazomegewa na si kukaa kutegemea umatonya nk
vigezo ni vingi lakini tujadili mada kwa hoja
 
Nakubaliana na mtoa hoja kwa kiasi kikubwa hapa dodoma Ignorance ni kubwa sana,ila kusema kuwa hapa viongozi wanachaguliwa kwa ukabila natofautiana nae,kwani Tanzania yote bado tunachagua viongozi hasa wabunge kwa Ukabila zaidi! Mfano hata mikoa ambayo wamesoma sana ukabila unatumika kama kigezo cha kupata viongozi,mfano Kilimanjaro,Kagera na Mbeya! Na kwingineko hivyo hivyo ni ukabila tu!!
 
Umeukomboa mkoa wako kwanza?ebu niambie mkoa gani tz umesalimika na umaskini hali ya tz inafanana kwa kiwango kikubwa ebu nionyesh mkoa gani tz hauna shida ya maji,afya,elimu etc wote tuko kwenye struggle mojatutafute ukombozi kwa tz nzima

kila mkoa una matatizo ila kuna kuzidiana!
Dodoma umezidi kwa matatizo jamani tuwe wa kweli tuu.
 
Back
Top Bottom