Waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi wakamatwa na Polisi mkoani Shinyanga

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limedai kuwakamata waganga wa Jadi 19 ambao wamekuwa wakipiga ramli chonganishi na kusababisha kuendelea kuwepo kwa matukio ya mauaji ya wananchi ambayo yamekuwa yakitokana na imani potofu za kishirikina.

Hayo yamebainishwa leo Machi 30,2019 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema katika misako mbalimbali ambayo inaendelea kufanyika na jeshi hilo ili kukabiliana na uhalifu pamoja na kupunguza mauaji yatokanayo na imani potofu za kishirikina, wamefanikiwa kuwakamata waganga hao 19 pamoja na watuhumiwa wengine 16 wakiwa na vitu vya wizi na madawa ya kulevya.

“Waganga hawa wa jadi tumewakamata pia wakiwa na nyara za serikali ambazo hutumia kupigia ramli chonganishi ambayo ni mikia ya nyumbu, ngozi ya kenge, ngozi ya simba, kucha za simba, mayai ya mbuni, kichwa cha kenge, jino la ggiri, pamoja na bundi mmoja ambaye tukimtoa hapa atakimbia,”amesema Kamanda Abwao.

“Pia katika msako mwingine tumefanikiwa kukamata watuhumiwa saba (7) wakiwa na mali za wizi ambazo ni pikipiki 2, mashine 3 za kunyolea saluni za kike, Tv 5, Radio Sabwoofer 5, Deki 5, King’amuzi kimoja, komputa moja, Friji moja, baiskeli 3, pamoja na watuhumiwa wengine tisa (9) wanawake wakiwa na madawa ya kulevya aina ya bangi uzito wa kilogramu 35 na heroine gramu 195,”ameongeza.

Aidha Kamanda amesema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za Kisheria, ili liwe fundisho kwa watu wengine ambao hawataki kuzitii sheria za nchi.

Pia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa dhidi ya waharifu, wakiwamo na wanganga wa jadi ambao wamekuwa wakitoa tiba kwa kupiga Ramli Chonganishi, ili mkoa ubaki kuwa salama kwa kudumisha amani na utulivu
PIKI%20WIZI.JPG
WIZI.JPG
MATUNGULI%202.JPG
BANGI.JPG
ONYESHA%20DHANA.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom