donniebrasco
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 887
- 775
Assalaam Aleykum,
Nchini Marekani magereza yana mfumo wa ufundishaji mbwa ambao unafanywa na wafungwa ndani ya magereza.
Mfumo huo umesaidia sana kupata mbwa wazuri kwa sababu ya muda mwingi unaotumika kuwafundisha kwa maana mfundishaji mmoja kwa mbwa mmoja ( mfungwa mfundishaji na mbwa wanakuwa karibu muda wote wako pamoja kwa miezi kadhaa ).
Wafungwa husika hupewa mafunzo vizuri sana juu ya ufundishaji na malezi ya mbwa.
Mbwa wengi wanakuwa na uelewa mzuri sana na wengi hutumika kusaidia viwete na vipofu.
Wafungwa wameonekana wakifurahi sana na kuwa na matumaini hata mara baada ya kukata tamaa, mbwa hao wamekuwa rafiki zao sana.
Na pia takwimu zimeonesha wafungwa wengi waliokuwa wakijihusisha na ufundishaji wa mbwa hawajafanya tena makosa makubwa walivyorudi uraiani baada ya kumaliza kutumikia muda wao gerezani.
Pia magereza yenye mifumo hii imeonekana hayana vurugu sana baina ya wafungwa kwa kuwa wamekuwa wakishughulika sana na mbwa.