Wafunga ofisi za Tanesco wakishinikiza mishahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafunga ofisi za Tanesco wakishinikiza mishahara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Dec 23, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  WALINZI wa kampuni moja ya ulinzi iliyoingia mkataba wa kulinda ofisi za Tanesco wilayani Muheza, juzi walifunga kwa kufuli, lango kuu la kuingilia katika ofisi hizo, wakiinikisha kampuni hiyo, iwalipe mishahara yao.

  Tukio hilo lililotokea mapema asubuhi, lilisababisha wafanyakazi wa Tanesco, kukaa nje ya ofisi kwa saa kadhaa.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizo katika eneo la tukio, mkuu wa walinzi katika katika kituo hicho, Asha Kihiyo, alisema uamuzi wa kufunga lango kuu la Tanesco, lililenga kuishinikiza kampuni yao iwalipe mishahara ya miezi miwili iliyopita.

  Kihiyo alisema kampuni hiyo haijawalipa mishahara yao kwa kipindi hicho, jambo linalowafanya wao na familia zao kuishi maisha magumu.

  "Tumechoka kuvumilia, watoto wanateseka kwa njaa na wengine wanashindwa kwenda shule kwa sababu hawajalipiwa ada," alisema.

  Alisema mara kadhaa wamejaribu kuwasiliana na viongozi wao, lakini hawatoi majibu yenye matumaini kuhusu mishahara yao.

  Alisema hali hiyo ndiyo iliyowasukuma kufunga lango kwa kutumia kufuli, ili kuwashindikiza viongozi hao kulipa mishahara hiyo ambayo alisema ni haki yao.

  Pia aliezea kusikitishwa kwake juu ya hatua ya kampuni hiyo, kuendelea kuwafanyisha kazi bila mikataba maalum ya ajira.

  Meneja wa Tanesco wilayani Muheza,Edward Mwakapuje, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata hivyo aliwasihi walinzi hao kufungua lango ili kuruhusu wafanyakazi kuingia katika ofisi zao.
  Alisema walinzi hao walimsikiliza na kukubali kufanya hivyo na kuwawezesha wafanyakazi wa Tanesco, kuendelea na shughuli zao.

  Mwakapuje pia alisema tatizo la walinzi hao, atalifikisha kwa Meneja Mkuu wa Tanesco wa Mkoa Tanga, ili naye awasiliane na uongozi wa kampuni hiyo ya ulinzi, kuhusu namna ya kulipatia ufumbuzi.
   
Loading...