Wafugaji, Watotoleshaji na Wauzaji wa kuku na samaki mnaombwa kuleta matangazo ya biashara zenu

Mtumwa baniani

Senior Member
Apr 13, 2013
128
26
Habari gani wakuu?

Napenda kuwataarifu kuwa tumeandaa chapisho tunalotegemea kuliingiza mitamboni ndani ya siku chache zijazo kuhusiana na ufugaji wa Kuku na samaki.

Kutokana na machapisho yetu kusomwa na watu wengi hapa Tanzania na katika nchi za Afrika Mashariki pamoja na mwamko wa watu katika swala la ufugaji huu,tunapata maombi mengi ya watu wanaotaka kuunganishwa na watu wanaotoa huduma zinazohusiana na ufugaji huu.

Kutokana na hilo tumeona tuwaletee fursa hii wafugaji wadogo na wakubwa kuzitangaza biashara zao kwa gharama nafuu sana nao watafaidika kwa kuunganishwa na masoko ya Afrika mashariki yote.

Kama wewe ni mfugaji, mtotoleshaji au muuzaji wa biashara tajwa hapo juu, tunakukaribisha ulete tangazo lako ili tuweze kukuwekea katika chapisho letu uweze kutambulika.

Gharama za kila tangazo ni sh. 50,000/= za Kitanzania tu na utapata nafasi ya kuitangaza biashara yako katika eneo zima la Afrika mashariki mpaka vijijini kusikofikiwa na huduma za internet. Pia utapata nafasi ya kuwekwa katika machapisho yetu mengine yanayohusiana na kilimo kwa kurudiwa kwa muda wa miaka 2 na kupewa nakala moja ya kila kitabu kilicho na tangazo lako.

Tunakaribisha pia matangazo kutoka kwa makundi haya:

Mafundi wa mabanda ya kisasa ya kufugia kuku wa kienyeji na wale wa kisasa.

Mafundi na wataalamu wa kujenga mabwawa ya Samaki wa kufuga.

Wazalishaji wa vyakula vya kuku.

Wauzaji wa vyakula vya kuku.

Wauzaji wa madawa ya kuku.

Wazalishaji wa vyakula vya samaki wa kufugwa.

Wamiliki wa maeneo yanayoweza kufaa kutumika kufugia samaki ambao wangependa kuingia ubia na watu walio na mitaji ya kufugia samaki.

Wamiliki wa maeneo yanayofaa kwa ufugaji wa samaki ambao wanayauza maeneo yao.

Wataalamu wa ufugaji wa samaki kwa ujumla na wale wanaojishughulisha na mambo yanayohusiana na biashara hizi kwa namna moja ama nyingine.

Kwa wenye kuhitaji huduma hii, tafadhali tuonane PM. Au unaweza kutuandikia katika email yetu : globalcorporatec@gmail.com

Karibuni sana.
 
Back
Top Bottom