Wafugaji holela wa kuku tukutane hapa!

No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,663
7,737
images(1).jpg
Hatuna presha wala hofu asbh tukiamka kazi kubwa kufungua tu mlango kuku hao wanasepa zao jioni wakishaingia tunafunga,hatujui kinga wala tiba hatujawahi kununua chochote dukani kwa ajili ya kuku wanaumwa wanapona wakizidiwa tunachinja ila hawaishi miaka nenda rudi bado tunao na wenyewe wana msimu kama wa embe tu. kwani mi nataka kuuliza nyie mnaofuga kwa kufuata wataalamu kuku wenu hawafi?kila kitu wataalam siku hizi hiyo miradi yao wapeleke huko sasa hivi nafikiria kuwa mfugaji mkubwa bila kutumia wataalam ntaweza tuu mambo gani haya mpaka kuku awe na daktari nae.
 
Kwanza nicheke
Ok, kila kitu namna kinavyotakiwa kufanywa au namna unavyokifanya inategemea na MALENGO yako ulijipangia, kuna wengine wanapenda tu "kuishi na kuku" (sio kufuga) sasa kwa wenzako kama hawa wanaopenda kuishi na kuku Daktari wa kazi gani? Awape chanjo au dawa ili iweje? Wao furaha yao ni kuona tu kuku wanazurura zurura pale nyumbani, watu wa aina hii mara nyingi hua hawana stress hata kuku akionyesha dalili za kuugua tiba wanayoijua ni moja tu KUCHINJA!

Kwa wale wenzang na mimi wanaofuga hasa kibiashara hawa sasa ndo wasije wakafuata ushauri wa bwana mkubwa pale wataumia na hata ule mtaji waliowekeza hautarudi kama unafuga kibiashara Chanjo, dawa, virutubisho gharama za Daktari HAZIEPUKIKI!
 
Hahahah eti mpk kuku awe na daktari , mkuu unawaonea wivu kuku eh ?
 
Kama hao kuku wanajitegemea wenyewe wewe sio mfugaji wa kuku, ni kuwa hao kuku wanakaa kwako, ni kama mtu ana mmbwa nyumbani lakini hajawahi mnunulia chakula hata siku moja mbwa anakula majalalali tu, huwezi sema kuwa unafuga mbwa ila nikuwa mbwa anaishi kwako.
 
Kama hao kuku wanajitegemea wenyewe wewe sio mfugaji wa kuku, ni kuwa hao kuku wanakaa kwako, ni kama mtu ana mmbwa nyumbani lakini hajawahi mnunulia chakula hata siku moja mbwa anakula majalalali tu, huwezi sema kuwa unafuga mbwa ila nikuwa mbwa anaishi kwako.
Sijawanyima msosi mimi wanakula.vizuri tena wananenepa kuliko hao wa madaktari wenu nimesema hao madaktari wenu siwataki kwa kuku wangu bora nitumie hata muarobaini sitaki hata kuwasikia madaktari wa kuku,wanaweka sumu kwenye kuku wanguu ntatumia mwarobaini mwanzo mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom