Wafuasi wa Kiongozi wa Upinzani Cameroon, Issa Tchiroma walinda nyumba yake wakihofia atakamatwa na Rais Paul Biya

Wafuasi wa Kiongozi wa Upinzani Cameroon, Issa Tchiroma walinda nyumba yake wakihofia atakamatwa na Rais Paul Biya

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Baada ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 12 Oktoba nchini Cameroon, pande zote mbili chama tawala na upinzani zinadai ushindi, ingawa matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo

Katika jiji la bandari la Garoua, kaskazini mwa Cameroon, wafuasi wa kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma Bakary wamejipanga kulinda nyumba yake usiku na mchana, wakiwa na wasiwasi kwamba serikali ya Rais Paul Biya inaweza kuagiza kukamatwa kwake

Vijana wa Cameroon wameweka zamu kulinda eneo la nyumba ya Tchiroma, wakiwa na vifaa vya jadi kama marungu na vipande vya mbao, wakilenga kumkinga kiongozi wao baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 12, 2025

Hassana Tchiroma, ndugu wa Issa Tchiroma, amesema
“Tchiroma alichoshwa na lugha ya chuki inayotoka kwa watu wanaomzunguka Rais Biya.”

Baada ya uchaguzi wa Oktoba 12, maandamano yenye vurugu yalitikisa jiji hilo baada ya vijana waliokuwa katika maandamano ya kumuunga mkono Tchiroma kufukuzwa na polisi wa kupambana na ghasia

Hassana Tchiroma alieleza kuwa wananchi wenyewe ndio waliamua kumlinda kiongozi huyo

Hali bado ni tete katika jiji la Garoua, ambalo sasa linaonekana kuwa chini ya ulinzi mkali.
Issa Tchiroma Bakary alijitangaza mshindi kupitia hotuba kwa wananchi wa Cameroon kutoka nyumbani kwake usiku wa Oktoba 13, 2025

Soma pia Kiongozi wa Upinzani ajitangaza Mshindi wa Urais Cameroon, amuomba Rais Paul Biya akubali Matokeo

 
If you want peace, prepare for war.

Amaini haiji bali kwa ncha ya upanga.

Wanadai haki wanaongea kama walevi wa ulanzi?
 
Back
Top Bottom