Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 345
- 307
Nimekuwa nikitafakari hali ya kisiasa nchini hususan mambo yanayotokea katika chama kikuu cha upinzani kwa sasa hususan imani na matendo yanayofanywa na wanachama na wshabiki wao.
Nikianza na matukio ya kuwachukulia watu walio tofauti nao kuwa ni wasaliti wasio na uwezo wa kuongoza au kufanya jambo katika ulimwengu wa siasa.
Leo hii mtu anaweza kuwa bora zaidi ndani ya chama hicho na akapewa sifa zote za uungwana anaostahili mtu,anaweza akapambwa kwa kila sifa kwa kuwa yupo ndani ya chama,lakini mtu huyo huyo ambaye leo anaonekana shujaa ndani ya chama kesho anapokuwa nje ya chama unaweza ukasikia madhaifu yake kutoka kwa wale waliokuwa wakimsifu mpaka utashangaa ni namna gani waliweza kuishi naye na kumsifu kabla.
Hali hii kwa washabiki na wanachama kuamini aliye katika nafasi wanayoitaka ndiye bora na akitoka nje ule ubora wake hupotea ni kosa kubwa katika mustakabali mzima wa ushindani wa kisiasa, inaweza ikajenga hisia ya kuwa wote walio katika chama ni wabovu na kinachofanyika ni kusitiriana ili kufika wanapotaka kwenda.
Pia kushindwa kutafuta sababu ya kwanini tuliokuwa nao wanaondoka na kujipa matumaini kuwa kuondoka kwao si tatizo hilo ni tatizo lingine katika ujenzi wa umoja kwani tukumbuke mfano huu mmoja wa Nabii Issa (Yesu) kwamba mchungaji yupo tayari kuwaacha mbuzi 99 walio zizini salama na kwenda kumtafuta mmoja aliepotea na atakapomkosa masikitiko yake huwa ni makubwa.