Wafiwa wazua kizaazaa hosptali wakidai maiti yao imeuzwa

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Wafiwa wazua kizaazaa hosptali wakidai maiti yao imeuzwa
Na Geofrey Nyang'oro

VURUGU kubwa zimeibuka jana katika Hosptali ya Manispaa Temeke Jijini Dar es Salaam, baada ya mwili unaodhaniwa kuwa wa marehem Bakari Omari uliozikwa kimakosa juzi kwenye makaburi Wailesi kubainika kuwa siyo wenyewe baada ya kufukuliwa.


Mwili huo ambao ulipotea katika mazingra ya kutatanisha ulifukuliwa jana katika makaburi hayo na kurudishwa katika chumba cha maiti ili ukatambuliwa ndugu zake.


Licha ya watu waliouchukua mwili huo kukiri kuwa maiti hiyo siyo ya ndugu yao, Joseph Antony aliyefariki na kuzikwa Oktoba 19 mwaka huu pia ndugu wa Omari Bakari waliukataa mwili kuwa siyo wa ndugu yao.


“Mwili wa ndugu yetu siyo huu, ndugu yetu hakuwa mzee tunataka uongozi wa hosptali hii utuletee mwili wa ndugu yetu Bakari Omari, ili tukamzike nyumbani kwetu Lushoto," alisema Ramadhani Mbwana.


Walisema wana wasiwasi mwili wa ndugu yao umeuzwa na baadhi ya watendaji hospitalini kwa watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya ili wakautumie kusafirishia dawa hizo.


Kauli hiyo iliyoamsha hasira ya ndugu hao na kuanza kufanya fujo ikiwa ni pamoja na kuvamia chumba cha kuhifadhia maiti na kumtoa nje mfanyakazi wa chumba hicho kuanza kupiga kwa ngumi mateke na mawe na kumjeruhi mguuni.


Mfanyakazi huyo, Mohamedi Jongo pia alinyang'anywa simu yake ya mkononi kabla ya kuokolewea na polisi wakishirikina na raia wema.


Katika sakata hilo lilishuhudiwa na umati mkubwa wa watu wafanyakazi wawili wa hospitali hiyo walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na ndugu wa marehemu huyo.


Mwili wa marehemu Bakari Omari ulipotea kwenye mazingra ya kutatanisha katika hospitali hiyo baada ya kuletwa hapo Oktoba 18, mwaka huu ukitokea Mbagala ambapo ilidaiwa kuwa alifariki ghafla Oktoba 17.


Oktoba 20 ndugu wa marehemu walikwenda hospitalini kuuchukua mwili huo ili kuupeleka nyumbani kwao Tanga kwa mazishi na kugundua kuwa ulikuwa umetoweka.


Baada ya kuelezwa hivyo ndipo uongozi wa hostali hiyo ulipowatambua watu waliochukua mwili huo na kuwaita polisi ili kuja kuthubitisha kama mwili waliouzika ulikuwa wakwao au la.


Watu hao walikuja na kukuta mwili wa ndugu yao, Joephu Antoniy ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.


Taarifa zilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Chang'ombe ndipo walipoitwa watu waliodaiwa kuchukua mwili huo na kwenda kuzika na kwamba watu hao walikiri kuwa waliuzika mwili ambao haukuwa wa ndugu yao.


Kutakana na tukio hilo la kusikitisha suala hilo lilipelekwa katika mahakama ya mwanzo Temeke na baada ye katika mahakama ya wilya ya Temeke kwa nia ya kupatiwa kibali cha kufukua mwili huo.


Jana majira ya saa saba mchana Mahakama ya Wilaya ya Temeke ilitoa kibali kilichoiamuru Manispaa ya Temeke kufukua mwili huo na kuurudisha hosptalini ili wafiwa wakautambue na kama ni wa ndugu yao wauchukue.


Kibali hicho kilitolewa na mwili wa marehemu ukafukuliwa na kurejeshwa hospitalini na wahusika wakaitwa kwa ajili ya kuutambua.


Hali ilibadilika baada ya Kinga Bakari, ambaye ndiye kaka wa marehemu kutoka nje ya chumba hicho kuwambia ndugu mwili huo siyo wa ndugu yao.


"Mimi namfahamu ndugu yangu hakuwa amezeeka hivi tunataka watuonyesha ndugu yetu walikompeleka,” alisema.


Ndipo ndugu walianza kumpiga mtumishi wa chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kumtoa nje kwa nguvu.


Mlinzi wa Hosptali hiyo wa kampuni ya SGS Kusila Hezeroni naye alijikuta akiambulia kipogo kikali kutoka kwa wafiwa hao alipokwenda kumsaidia Jongo aliyekuwa ameangashwa chini.


Hezeron alinyang'anywa rungu lake na kuanza kupigiwa nalo yeye mwenye mpaka alipojiokoa na kukimbilia katika jengo la ofisi za utawala


Vurugu hizo za aina yake ziliwalazimu wafanyakazi, wagonjwa na watu waliokuwa katika eneo la hilo kukimbia huku na kule ili kujificha.


Polisi waliwasili katika eneo hilo waliwakamata watu wanne wakiwamo wanawake wawili kwa kwa madai ya kufanya fujo hospitalini.


Akizungumzia tukio hilo Mganga Mkuu wa Hosptali hiyo Dk. Asha Mahita alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mwili wa Bakari ndiyo huo..


Alisema waliosema mwili siyo wa ndugu yao kwa sababu hawajui kwamba baada ya mwili kukaa muda mrefu chumba cha maiti huvimba.
 
Back
Top Bottom