[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 546"]
[TR]
[TD="width: 92%"] TAKUKURU yawahoji watuhumiwa TTCL
[/TD]
[TD="width: 2%"] [/TD]
[TD="width: 2%"] [/TD]
[TD="width: 2%"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 590"]
[TR]
[TD="width: 787"] Imeandikwa na Edmund Mihale, Dar es salaam
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 787"] Jumanne, Januari 29, 2013 16:20
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 787"] Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeanza rasmi kazi ya kuwahoji viongozi juu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Wanaotuhumiwa na kuchunguza na TAKUKURU ni Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Amir Said, Mkurugenzi wa Fedha, Mrisho Shabaan na maafisa wengine waandamizi. Kati ya tuhuma zinazowakabili ni matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji fedha na mkakati wa makusudi wa chini kwa chini wenye lengo la kuiangamiza TTCL kwa faida ya kampuni binafsi. Hatua ya kuwafikisha mbele ya TAKUKURU imekuja baada ya JAMHURI kuripoti ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka uliofanywa na viongozi hao. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba aliitisha mkutano na wafanyakazi wa shirika hilo wiki iliyopita na kuamua malalamiko ya wafanyakazi yashughulikiwe na TAKUKURU. Pia Makamba imeitaka Bodi ya TTCL kukaa na kumwandikia barua Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya kukagua hesabu za shirika hilo la umma. Chanzo cha kuaminika ndani ya TTCL, kimeliambia JAMHURI kuwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Karim Bablia tayari amehojiwa na TAKUKURU kwa nia ya kufafanua shutuma nzito alizomwaga hadharani katika kikoa kati ya wafanyakazi na Makamba. Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi wa menejimenti ya TTCL wameandaa taarifa zitakazotumika kuwahadaa watumishi wa TAKUKURU kama njia ya kukwepa mkono wa sheria. Tumepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi tayari amepigiwa simu na TAKUKURU kwa ajili ya kuhojiwa na chombo hicho. Sasa tumeamini kuwa Serikali inafanya kazi kwani tuliambiwa kuwa baada ya kumaliza mkutano Naibu Waziri aliwaita TAKUKURU na kuwakabidhi makabrasha yenye malalamiko yetu nao wameanza kuwaita wahusika, kimesema chanzo kingine. Katika mkutano huo, Makamba alitaka manejimenti ya Shirika hilo kuitisha kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kilichotarajiwa Alhamisi iliyopitakupitisha mapendekezo ya wafanyakazi. Wafanyakazi katika mapendekezo hayo walitaka kufanyika kwa ukaguzi wa hesabu kupitia Ofisi ya CAG jambo ambalo Bodi haijalifanya kutokana na kikao hicho kuahirishwa baada ya idadi ya wajumbe inayotakiwa kutotimia siku ya Alhamisi. Wajumbe wa Bodi hiyo waliokosekana ni Mwakilishi, Detecom na MSI, Jaji Joseph Warioba na Mkurugenzi wa Benki ya Mkombozi, Edwina Lupembe. Makamba katika mkutano huo amesema wote watakaobainika kutumia madaraka vibaya wakati wa uongozi wao watashitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. Amesema wizara yake tayari imeanza mchakato wa kutafuta menejimenti mpya itakayoongoza shirika hilo ndani ya wiki mbili baada ya kubaini iliyopo haifai. Huwezi kuwa na menejimenti yenye uhusiano mbaya na wafanykazi wake hata tukiamua kuingiza bilioni 180 hapa zitakwisha kwani wafanyakazi na menejimenti hawaheshimiani. Zitakwisha zote hivyo ninawahakikishieni kuwa tutakapoonana wiki mbili au tatu zijazo tutakuwa na uongozi mpya, amesema Makamba. Hata hivyo, Makamba amesema Serikali iko katika mazungumzo na wawekezaji walipo TTCL inunue hisa zote na kumiliki shirika hilo kwa asilimia 100. Madai ya Wafanyakazi Akichangia katika mkutano huo, Meneja wa Mkoa wa Kaskazini, Karim Bablia amesema kuwa katika kanda yake kwa miaka miwili sasa ametakiwa kukusanya Sh bilioni 4.7 ila akavuka lengo na kufikia Sh bilioni 7.9 lakini kila mwaka katika makusanyo kumekuwa na upotevu wa Sh bilioni tatu. Bablia amesema ametumia mbinu mbalimbali kufuatilia upotevu huo lakini uongozi wa juu umekuwa ukimkatisha tamaa kwa kutoa majibu ya jeuri. Nasema hapa hakuna kitu kibaya kama unapewa bajeti unakusanya na kuvuka lengo waliokuwekea, lakini ripoti inayoletwa katika kikao cha mameneja unaambiwa kuwa Sh bilioni 3.5 [kati ya hizo] hazionekani, unauliza unajibiwa kijeuri, hii Mheshimiwa Waziri inakera sana. Nimefuatia katika kila idara kupata ukweli wa upotevu huu kwa miaka miwili sasa, lakini napigwa danadana ukifuatilia sana unapewa majibu ya kejeli unambiwa wewe ndo unapenda shirika sana, amesema Babilia. Amesema shirika hilo lina nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika soko, lakini linakwamishwa na menejimenti iliyopo. Msheshimiwa Waziri hadi sasa nimepeleka maombi ya modem 600 zinazohitaji kwa wateja nimeambiwa hadi wiki sita hivi. Haya niliomba dola 2000 kwa ajili ya kuwafungia simu wateja wetu wakubwa . ni ni ni nani hawa ok .. Benki ya CRDB, lakini naambiwa kuwa dola hizo hazipo. Jamani shirika hili linakwenda wapi? Hadi sasa hawajafungiwa simu hizo wako katika foleni. Katika kanda yangu nina wateja 3,600, lakini mtambo uliopo una uwezo wa kuchukua wateja 1,800 sasa nimepiga kelele kwa menejimenti, lakini wameweka pamba masikioni kwa mtaji huu tutaliokoa shirika hili kweli? Wateja wapo tunashindwa kuwahudumia kwa kushindwa vitu vidogo vidogo tu. Lakini haya yote nayafanya menejimenti inaniona kuwa sifai baadala yake naambiwa kuwa mie natoa siri ya shirika katika magazeti ninasema mimi ninaijua kazi yangu. Kila ninachokifanya nataarifu viongozi wangu mameneja. Machifu jamani, mameneja wenzangu ni uongo? Kama ni uongo mtu asimame hapa na kukataa kama ni uongo. Kila mtu humpa taarifa ya kile ninachodai. Sina haja ya kupeleka katika magazeti mambo ya ofisi. Lakini Mheshimiwa Waziri yaliyoandikwa kwenye gazeti sitaki kulitaja ni gazeti lipi hapa [akimananisha JAMHURI] ni kweli tupu. Hakuna hata chembe ya uongo. Kuna kampuni imepewa kazi ya kulinda katika kanda yangu na nyingine hawana askari. Hata akiwepo, hana silaha yeyote. Kila siku mie ni mtu wa kwenda kutoa ripoti polisi inayohusu wizi. Sasa nina RB zaidi ya 20. Menejimenti imekaa kimya, tumelalamika tumeshindwa kupata majibu, amesema. Akiwasilisha madai kwa niaba ya wafanyakazi, Lucas Ishengoma amesema uongozi wa menejimenti umeshindwa kufanya kazi sasa umebaki kula fedha. Makamba baada ya kupokea tuhuma hizo nzito aliamua kuzikabidhi TAKUKURU bila kuwapa fursa ya kusikilizwa viongozi wakuu wa TTCL akisema ikiwa wanalo la kujitetea watalitoa mbele ya TAKUKURU. JAMHURI kwa muda wa mwezi mzima sasa limekuwa likiripoto wizi, uozo na uzandiki unaondelea ndani ya TTCL hali inayolibemenda shirika hilo kongwe la simu nchini. [/TD]

[TD="width: 100%"] Bosi TTCL ashinikiza mkataba wa mamilioni
[/TD]
[TD="width: 100%"] [/TD]

[TD] Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Jumanne, Januari 08, 2013 14:12
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] *Asaini huku akijiandaa kungatuka kazini *Kampuni ya ulinzi yabainika utata mtupu *Walinzi wake watuhumiwa wizi wa mali
MKATABA tata wa Sh milioni 742 kati ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Kampuni ya Ulinzi ya Supreme International Limited, umeanza kuwatokea puani viongozi wa TTCL, JAMHURI imethibitishiwa.
Mkataba huo ulisainiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa TTCL, Said Amir, Mei 14, mwaka jana; wakati muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria ukiwa ni Agosti 30, mwaka jana. Licha ya muda wake wa utumishi kumalizika, bado anaendelea kushikilia wadhifa huo. Muda wa kwisha kwa mkataba huo ni Aprili 30, 2015.
JAMHURI imefanikiwa kupata baadhi ya nyaraka zinazoonyesha kwamba baadhi ya viongozi ndani ya TTCL walipinga kampuni hiyo kuingia mkataba wa ulinzi na Supreme, lakini uongozi wa juu ulishinikiza na kufanikisha mpango huo.
Hoja ya kupinga mkataba baina ya kampuni hizo mbili ilijikita kwenye utata wa Supreme International Limited, hasa kwenye suala la mahali zilipo ofisi na kama kweli kulifanyika ukaguzi kujiridhisha kama ina uwezo wa kufanya kazi ya kulinda TTCL.
Utata mwingine wa mkataba huo upo kwenye idadi ndogo ya walinzi wanaoshiriki ulinzi kwenye vituo wanavyopangiwa, tofauti na idadi inayoonyeshwa kwenye mkataba.
Taarifa zinasema pia kuwa kampuni ya Supreme haina vitendea kazi kama bunduki, jambo linalosababisha kuwapo hatari ya usalama wa mali za TTCL.
Pia kuna tuhuma kuwa baadhi ya walinzi wa kampuni hiyo si waaminifu kwa mujibu wa matukio ya karibuni yaliyoripotiwa katika vituo vya Masaki, Ubungo Maziwa, Magomeni, Oysterbay na Sinza.
Historia ya mkataba/utata idadi ya walinzi
Ulisainiwa Mei 14, mwaka jana kati ya Said Amir, akiwakilisha TTCL; na Mkurugenzi Mtendaji wa Supreme International Limited, Deogratias Muganda; na kushuhudiwa na mwanasheria aliyejitambulisha kwa jina la Anita Samwel Mushi. Muganda ameitambulisha Supreme International Limited kuwa inapatikana kupitia Sanduku la Barua 61614 Dar es Saalam. Anuani hiyo hiyo pia ndiyo inayotumiwa na kampuni yake nyingine ya Utdager Consultant and Business Investment ya Dar es Salaam.
Utata unajitokeza kwenye idadi ya walinzi ambao kampuni hiyo inapaswa kuwaweka kwenye vituo kama walivyofikia makubaliano na TTCL.
Kwa mujibu wa mkataba huo, kila kichwa kinapaswa kulipwa na TTCL Sh 180,000 kwa mwezi.
Imebainika kuwa katika vituo kadhaa, idadi ya walinzi si ile iliyoelezwa kwenye mkataba, hiyo ikiwa na maana kwamba kampuni inalipwa fedha nyingi kwa walinzi hewa.
Baadhi ya vituo ambavyo vinaonyeshwa kwenye mkataba kwamba wakati wa mchana vinapaswa kuwa na walinzi wawili, imebainika kuwa mlinzi mmoja tu hufanya kazi hiyo. Kwa usiku, baadhi ya vituo vinavyoonyeshwa kwenye mkataba kuwa na walinzi wanne, mara nyingi kampuni hiyo imekuwa ikipeleka mlinzi mmoja au wawili.
Kwa upande wa silaha, imebainika kuwa mkataba unaitaka kampuni hiyo iweke walinzi 113 kwa mgawo kulingana na kanda tatu za Dar es Salaam Kati, Dar es Salaam Kaskazini na Dar es Salaam Kusini.
Kwa mchanganuo huo, malipo kwa Dar es Salaam Kati yanapaswa kuwa Sh 99,000,000 (walinzi 15); Dar es Salaam Kusini Sh 212,760,000 (walinzi 32); na Dar es Salaam Kaskazini Sh 431,280,000 (walinzi 66).
Kwa idadi hiyo, malipo yanapaswa yafanywe kwa askari 113, lakini JAMHURI imejiridhisha kuwa kampuni hiyo haina idadi hiyo ya askari wanaopelekwa kwenye malindo. Hii ina maana kwamba fedha nyingi zimekuwa zikiishia mikononi mwa kampuni hiyo ya ulinzi pamoja na maofisa kadhaa wa TTCL.
Said amekuwa hataki kutoa ushirikiano kwa JAMHURI. Mara kadhaa anapopigiwa simu, amekuwa akikata baada ya mwandishi kujitambulisha. Hata anapopelekewa ujumbe mfupi wa maandishi, amekuwa hajibu. Hali ni hiyo hiyo kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Mrisho Shabani ambaye hataki kupokea simu.
Wamiliki wa Supreme International Limited
Kwenye usajili kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inaonyesha kuwa makazi yake ni mkoani Mwanza. Ilisajiliwa Novemba 24, 1995 kwa namba 38363; na kufanyiwa marekebisho ya usajili mwaka 2009.
Katika anuani yao, Supreme inaonyesha kuwa mdhamini wake mkuu ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Ilianza kwa mtaji wa Sh 30,000,000 kwa kila mwanahisa kuwa na hisa 3,000 zikiwa na thamani ya Sh 10,000 kila moja.
Wanahisa hao ni Charles Kazana Munubi anayemiliki hisa 1,000; Utdager Consultant and Business Investment Limited inayomilikiwa na Deogratias Gabriel Muganda (1,000) na Vedastus Kalwizara Lufano (1,000).
Wakurugenzi wa kampuni hiyo ni Charles Kazana Munubi anayepatikana kupitia Sanduku la Barua 7657, Mecco Kitalu FF kiwanja Na. 522 Nyakato, Mwanza; Utadger Consultant and Busness Limited Sanduku la Barua 61614; Kiwanja Na. 520 /A, Sinza, Dar es Salaam.
Mwingine ni Vedastus Kalwizira Lufano anayepatikana kupitia Sanduku la Barua 7657, Mecco Kitalu FF, Kiwanja Na. 520 Nyakato, Mwanza.
Katika Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika Machi 10, 2005 uliamua kumuongeza mwanahisa mwingine, Deusdet David Muhanuzi aliyenunua hisa 3,000 kwa thamani ya Sh 10,000 kwa kila hisa; hivyo kuifanya kampuni kuwa na wakurugenzi wanne.
Kwa mujibu wa BRELA, kampuni hiyo haijapeleka taarifa za marejesho yake ya mwaka kwa miaka 10 sasa kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka jana. Taarifa nyingine zinasema kwamba Supreme imewasilisha taarifa hizo, lakini zina upungufu.
Hata hivyo, uchunguzi wa Jamhuri umebaini kuwa Supreme imepata mikopo kutoka benki mbalimbali za hapa nchini. Imekopa kutoka NMB, CRDB, Kenya Commercial Bank; na mkopo wa karibuni kabisa waliupata kutoka Barclays ambako walipata Sh milioni 120 mnamo Oktoba 29, mwaka jana, ingawa hawajawasilisha taarifa hizi BRELA. [/TD]

[TD="width: 100%"] JAMHURI yaisafisha TTCL

[TD] Imeandikwa na EMUND MIHALE, DODOMa
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Jumanne, Februari 05, 2013 06:41
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imemngoa katika madaraka Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Said Amir, na kuwasimamisha kazi maofisa wengine watatu waandamizi ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi zinazowakabili. Kwa wiki kadhaa, JAMHURI imeandika kwa kina taarifa za matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi uliopindukia kwenye matumizi ya fedha za kampuni hiyo ya umma. Miongoni mwa mikataba hiyo ni ule wa Sh milioni zaidi ya 700 ambao uongozi wa TTCL, chini ya Amir uingia na kampuni ya ulinzi ya Supreme ilhali ikiwa haina walinzi wa kutosha, upungufu wa silaha na walinzi kadhaa wenye sifa za wizi ambao wana kesi polisi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Enos Bukuku; nafasi ya Amir imechukuliwa na Dk Kamugisha Kazaura. Mabadiliko hayo yameanza rasmi Februari mosi, mwaka huu. Miongoni mwa waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Fedha, Mrisho Shabani; Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Ernest Nangi; na Mkaguzi wa Hesabu za Ndani, Godfrey Kilenga. Pamoja na Dk. Kazaura, wengine walioteuliwa kukaimu nafasi mbalimbali ni Alinanuswe Mwakitalima (Kaimu Mkurugenzi wa Fedha);, Peter Ngota (Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Masoko); David Kalayi (Kaimu Mkaguzi wa Hesabu za Ndani), Jotham Lujara (Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi); na Mkurugenzi anayesimamia Mkongo wa Taifa, Adin Mgendi. Bodi imewataka wafanyakazi wawape ushirikiano viongozi hao wapya. [/TD]

[TD="width: 100%"] Ufisadi washamiri TTCL

[TD] Imeandikwa na EDMUND MIHALE, DAR ES SALAAM
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Jumatano, Januari 23, 2013 10:41
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] *Mabilioni ya makusanyo yayeyuka Wakati Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, January Makamba, alitarajiwa kukutana na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) jana, viongozi wakuu wake wanatuhumiwa kufanya ufisadi unaoiangamiza kampuni hiyo ya umma. Kila mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi analipwa Sh milioni moja kwa siku; hizo zikiwa nje ya marupurupu mengine. Wakati wajumbe wakitafuna mamilioni hayo, imebainika kuwa mamilioni ya shilingi hupotea kutoka kwenye makusanyo ya kanda, huku Dar es Salaam ikichukuliwa kama kitovu cha ufisadi huo. Chanzo cha habari cha uhakika kutoka ndani ya TTCL kimeiambia JAMHURI kuwa kwa sasa Kampuni hiyo imekuwa shamba la bibi kwa kuwa viongozi wa juu wameanzisha mtandao unaotafuna fedha za umma. Mkoa wa Kaskazini unaongoza kwa makusanyo ya fedha. Mwaka jana ulizalisha Sh bilioni 7.9. Lengo lilikuwa kukusanya Sh bilioni 4.8 kwa mwaka, lakini cha kushangaza katika kumbukumbu za TTCL Sh bilioni tatu hazionekani katika hesabu. Katika Mkoa wa Dar es Salaam Kati hesabu Makao Makuu ya TTCL Sh bilioni 3.5 nazo hazionekani katika hesabu, kimesema chanzo cha habari. Ufisadi huo umewashtua wafanyakazi, kiasi cha kutoa wito kwa uongozi wa juu kumtumia Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuichunguza kampuni hiyo. Wafanyakazi wanahoji uhalali wa kutumiwa kwa kampuni moja ya ukaguzi wa hesabu, huku baadhi ya viongozi wa TTCL wakiwa wameshawahi kufanya kazi katika kampuni hiyo ambayo ni ya kimataifa. Taarifa za ndani ya kikao kilichofanyika katika moja ya hoteli katikati ya Jiji la Dar es Salaam zinaeleza kuwa mameneja wa mikoa wametishia kuishtaki menejimenti hiyo wizarani iwapo haitatoa hesabu sahihi za makusanyo. Hata hivyo, kuna taarifa inadai kuwa Meneja Mishahara, Hamida Masoli, amekimbilia nje ya nchi baada ya Kitengo cha Usalama ndani ya kampuni hiyo (CIA) kubaini kuwa anamiliki akaunti yenye Sh bilioni moja. Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na wafanyakazi hao kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, fedha hizo zinadaiwa kuchukuliwa katika kampuni hiyo. Akijibu shutuma hizo, Mkurugenzi wa Idara wa Fedha, Shaban Mrisho, amesema kuwa tatizo katika kampuni hiyo ni uhusiano mbaya kati manejimenti na wafanyakazi. Amesema kamapuni hiyo imejaa siasa kwa kuwa wafanyakazi wamekuwa wakipeleka maneno katika vyombo vya habari hata yale yasiyo na ukweli ndani yake. Akijibu kuhusu manejimenti kula fedha za makusanyo, amesema hakuna fedha yeyote inayoliwa kwa kuwa hesabu zote ziko sawa bali wafanyakazi wanashindwa kuelewa kuwa hesabu hizo zimeunganishwa na Ongezeko la Thamani (VAT). Katika hesabu walizosema hawa watu wanashindwa kuelewa kuwa kuna mambo mengi pindi tunapowapangia malengo. Tunapopanga malengo huwa hakuna VAT, bajeti inakuwa nje na VAT, sasa wanapoleta hesabu zao huku lazima tulipe VAT ndio hapa sasa unaona kuwa kuna hela inazidi. Lakini katika hesabu hizo pia kuna makusanyo yanayotokana na mali za kampuni kama kodi za majengo nazo wanaingiza kwenye bajeti yao jambo ambalo ni kosa, huko wanatakiwa kukumbuka kuwa kodi zote za nyumba za kampuni katika maeneo yao zinaingia makao makuu. Tatizo siku zote linatoka katika Kanda ya Kaskazini huko ndio kwenye chokochoko, kuna watu wanajiita wanaharakati, meneja wao ndio mtu wa kwanza ambaye ameshindwa kuwasilisha bajeti lakini amekuwa wa kwanza kulalamika, jamani hatuwezi kuiba kupitia bajeti, amesema Mrisho. Akizungumzia wizi uliofanywa Masoli amekiri kuwapo kwa wizi huo lakini amekanusha kuwa si kwa kiwango kilichotajwa. Amesema kuwa Masoli alichoiba ni fedha kidogo ambayo alikuwa kwa ajili ya kununua mafuta, hata hivyo alishindwa kutaja ni kiwango gani alichoiba. Jamani huyu mama mie sijui kama amekimbia nchini lakini kiasi kinachotajwa ni kikubwa mno kwani amekuwa akichukua kidogo kidogo tangu mwaka 2007 ni hela ya mafuta tu au labda kama baba, mjomba au bibi walikuwa wanaumwa anachomoa kidogo hadi kimefika kiasi hicho, amesema. [/TD]

[TD="width: 100%"] Madudu mengine TTCL

[TD] Jumanne, Desemba 18, 2012 10:17
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] *Wasaini mkataba wa ulaji wa Sh milioni 740 kwa mwaka
*Walishirikiana na maofisa kuweka walinzi hewa lindoni
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imeingia mkataba wenye utata na kampuni moja ya ulinzi wenye thamani ya Sh milioni 742 kwa mwaka. Utadumu hadi mwaka 2015. Utata wa mkataba huo unatokana na idadi ndogo ya walinzi wanaoshiriki ulinzi kwenye vituo wanavyopangiwa, tofauti na ile inayoonyeshwa kwenye mkataba. Ulisainiwa Mei 14, mwaka huu, kati ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Said Amir, akiwakilisha TTCL; na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo yenye anuani inayoonesha kuwa ipo Dar es Salaam na Mwanza. Mkataba huo unaonyesha kuwa ulipaswa kuanza Mei Mosi, 2012 na kwisha muda wake Aprili 30, 2015. Utata unajitokeza kwenye idadi ya walinzi ambao kampuni hiyo inapaswa kuwaweka kwenye vituo kama walivyofikia makubaliano na TTCL. Kwa mujibu wa mkataba huo, kila kichwa kinapaswa kulipwa na TTCL Sh 180,000 kwa mwezi. Imebainika kuwa katika vituo kadhaa, idadi ya walinzi si ile iliyoelezwa kwenye mkataba, hiyo ikiwa na maana kwamba kampuni hiyo inalipwa fedha nyingi kwa walinzi hewa. Baadhi ya vituo ambavyo vinaonyeshwa kwenye mkataba kwamba wakati wa mchana vinapaswa kuwa na walinzi wawili, imebainika kuwa ni mlinzi mmoja tu anayefanya kazi hiyo. Kwa usiku, baadhi ya vituo vinavyoonyeshwa kwenye mkataba kuwa na walinzi wanne, mara nyingi kampuni hiyo imekuwa ikipeleka mlinzi mmoja au wawili. Kwa upande wa silaha, imebainika kuwa Mkataba unaitaka kampuni hiyo iweke walinzi 113 kwa mgawo kulingana na kanda tatu za Dar es Salaam Kati, Dar es Salaam Kaskazini na Dar es Salaam Kusini. Kwa mchanganuo huo, malipo kwa Dar es Salaam Kati yanapaswa kuwa Sh 99,000,000 (walinzi 15); Dar es Salaam Kusini Sh 212,760,000 (walinzi 32); na Dar es Salaam Kaskazini Sh 431,280,000 (walinzi 66). Kwa idadi hiyo, malipo yanapaswa yafanywe kwa askari 113, lakini JAMHURI imejiridhisha pasi na shaka kuwa kampuni hiyo haina idadi hiyo ya askari wanaopelekwa kwenye malindo. Hii ina maana kwamba fedha nyingi zimekuwa zikiishia mikononi mwa kampuni hiyo ya ulinzi pamoja na maofisa kadhaa wa TTCL. Said Amir wa TTCL, alipoulizwa hakutaka kuzungumzia wizi huu, badala yake ametaka JAMHURI iwasiliane na Mkuu wa Kitengo cha Fedha TTCL, Mrisho Shabani. JAMHURI iliwasiliana na Mrisho mara kadhaa, ambapo ametaka nakala ya mkataba aweze kujiridhisha. Pamoja na kupewa nakala na maswali kadhaa, hadi tunakwenda mitamboni, Mrisho hakuwa tayari kujibu. Mara ya mwisho alipopigiwa simu, alijibu kwa ujumbe wa maandishi akisema, Tuko mkutano wa wafanyakazi wote na mwenyekiti wa bodi. [/TD]