Wafanyakazi wawili wa BancABC wafikishwa mahakamani kwa wizi wa zaidi ya Milioni 23

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Wafanyakazi wa Benki ya BancABC Tanzania, wafikishwa mahakamani wakituhumiwa kuiibia benki shilingi 23,700,000.

Wawili hao waliotambulika kama Paul Mwakiteleko na Edward Kubagwa wanadaiwa kughushi nyaraka ili kupata pesa hizo. Wamefikishwa mahakama ya Samora, Kariakoo.
 
Pumbavu kweli.. Benki unaiba tumilioni tushna saba.... Kende kabisa
Soryy .. Kenge nilimaanishaa
Ulitaka waibe ngapi ndio uwasifu
So kila mtu kaiba 11mil,
Yaani wanaingia matatizoni, usubufu wa polisi & mahakama, kazi hakuna tena na aibu ya kuonekana wezi sababu ya 11mil tu??
Kweli aliesema "Ukitaka Kula Nguruwe basi Kula alienona" hakukosea
 
Wafanyakazi wa Benki ya BancABC Tanzania, wafikishwa mahakamani wakituhumiwa kuiibia benki shilingi 23,700,000.

Wawili hao waliotambulika kama Paul Mwakiteleko na Edward Kubagwa wanadaiwa kughushi nyaraka ili kupata pesa hizo. Wamefikishwa mahakama ya Samora, Kariakoo.
Hawa nao ni wajinga sasa 23m/=
Huu ujinga sasa
Si wangeiba hata 300m/=
Kama unataka kuiba iba pesa ndefu ya uhakika sio vijifedha kidogo hivyo.
Hawajufinzi kwa Escrow
Kesi imeisha hapo!!
 
Jamii inasifia wizi, uhalifu na ufisadi. Si uaminifu tena.
By the way wapo mahakamani, na hatuwezi kusema ni wizi. They are not guilty at the moment.
Hata hivyo kwa rasilimali za benki etc ni bora kuwafuta kazi au kuhangaishana mahakamani?
 
Waswahili hamkosi jambo wakiiba kiduchu mnawalalamikia wakipiga mshiko mnene ooh wafanyakazi wa benk hawafai. Mwizi ni mwizi, hata aibe senti tano au sindano haibatilishi uhalali wa tendo!
 
Naona vijana wanasifia wizi, wanataka watu waibe pesa nyingi. Nchi imeoza hii.
 
Back
Top Bottom